

Lugha Nyingine
Mbunifu aliyezaliwa baada ya miaka ya 90 "abadilisha" mabaki ya kitamaduni kuwa midoli ya kupendeza (2)
![]() |
Zeng Zhou akitambulisha midoli na sanamu mbalimbali alizokusanya kwa watoto wanaotembelea duka lake mjini Chengdu, Mkoa wa Sichuan, kusini-magharibi mwa China, Machi 1, 2025. (Xinhua/Wang Xi) |
Zeng Zhou, mbunifu wa bidhaa bunifu za kitamaduni na mwendeshaji mipango aliyezaliwa katika miaka ya 1990, amekuwa akivutiwa na bidhaa za katuni na filamu vilevile midoli iliyo kwenye fasheni pamoja na sanamu za maumbo mbalimbali tangu utoto wake, akiota kubuni bidhaa bunifu za kitamaduni zinazojumuisha haiba ya utamaduni wa jadi wa China.
Mwaka 2018, Zeng aliacha kazi yake katika kampuni ya michezo ya kompyuta na kuwa mbunifu wa kujitegemea. Akiwa amehamasishwa na kazi maarufu za kisanaa za shaba zikiwemo za Mti Mtakatifu (Sacred Tree), vinyago na nyuso za wanyama zinazoonyeshwa kwenye Jumba la Makumbusho la Sanxingdui, mkoani Sichuan, China, alibuni kazi nyingi bunifu za kitamaduni za kupendeza kwa kuzichanganya katika mambo ya kisasa yanayopendwa na watu. Kazi zake zimemletea tuzo nyingi katika mashindano ya kubuni.
Aidha, Zeng ameanzisha shindano la mawazo bunifu juu ya midoli ya kisanaa na amekuwa akiliendesha kwa miaka miwili mfululizo. Washiriki kutoka kote nchini China humiminika ili kuonyesha kazi zao na kubadilishana mawazo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma