Kujua demokrasia ya umma ya China ya mchakato kamili (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 04, 2025
Kujua demokrasia ya umma ya China ya mchakato kamili

Demokrasia ni thamani ya pamoja ya binadamu wote, na ni wazo muhimu linaloshikiliwa siku zote na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na watu wa China. Tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha CPC ulipofanyika mwaka 2012, kamati kuu ya Chama ambayo Komredi Xi Jinping akiwa kiini chake imefahamisha kwa kina kuhusu kanuni ya maendeleo ya siasa ya kidemokrasia ya China, ikitoa wazo la demokrasia ya umma ya China ya mchakato kamili na kulihimiza kwa nguvu.

Hivi leo, demokrasia ya umma ya mchakato mzima inaonesha ustawi na uhai mkubwa nchini kote China. Watu wa China wanaongeza imani zaidi juu ya mfumo wao wa demokrasia, na njia ya kidemokrasia yenye umaalumu wa China imekuwa pana zaidi. Katibu mkuu Xi Jinping amefahamisha kwa kina mara kwa mara sifa wazi na nguvu dhahiri za demokrasia hiyo ya umma ya mchakato kamili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha