

Lugha Nyingine
Timu ya madaktari wa China yatoa huduma za matibabu bila malipo kwa wazee wa Malta (5)
![]() |
Yang Libai (kulia), kiongozi wa timu ya 20 ya madaktari wa China nchini Malta, akitoa huduma za matibabu ya kijadi ya China kwa mwanamke mjini Santa Lucija, kusini mwa Malta, Februari 19, 2025. (Xinhua/Chen Wenxian) |
VALETTA – Timu ya 20 ya Madaktari wa China nchini Malta kutoka Kituo cha Kikanda cha Mediterania cha Matibabu ya Kijadi ya China imetoa huduma za matibabu bila malipo kwa wakaazi wazee siku ya Jumatano katika Bustani ya Utulivu ya China mjini Santa Lucija, kusini mwa Malta.
Yang Libai, kiongozi wa timu hiyo, alitoa mhadhara juu ya matibabu ya kijadi ya China (TCM), akielezea umuhimu wa matibabu ya kijadi ya acupuncture katika kutibu magonjwa ya kawaida kama vile shingo, sehemu ya chini ya mgongo, na maumivu ya mguu. Zaidi ya hayo, aliwaongoza washiriki wa shughuli katika kutambua sehemu muhimu za mwili za kutumia tiba hiyo, akielezea kazi na matumizi yake.
Shughuli ya majadiliano kwenye mhadhara huo ilivuta shauku kubwa, huku washiriki wengi walisema kuwa matibabu ya kijadi ya China ni ya ajabu na yenye kufikiwa. Kufuatia mhadhara wake huo, Yang alitoa vipimo vya shinikizo la damu na matibabu ya kijadi ya China ya kufanya masaji kwa washiriki.
Cettina, mwenye umri wa miaka 79, amesema kwamba mpwa wake aliwahi kufanyiwa matibabu ya acupuncture kutokana na ugonjwa wa wasiwasi, ambayo yalipunguza dalili zake kwa kiasi kikubwa.
"Siku zote nimekuwa na maoni mazuri kuhusu matibabu ya kijadi ya China," amesema, akiongeza kuwa alikuwa na hamu ya kujaribu mwenyewe matibabu hayo ya acupuncture, kwa kuwa amekuwa katika matatizo ya ugonjwa wa arthritis na uvimbaji wa viungo kwa miaka mingi.
“Shughuli imelenga kutambulisha utamaduni wa matibabu ya kijadi ya China kwa wakaazi zaidi wa huko kwa kutoa ushauri wa kiafya na huduma za matibabu bila malipo,” Yang amesema, akisisitiza kwamba shughuli kama hiyo itaendelea kufanywa ili kuongeza uelewa na utumiaji wa umma wa TCM.
MRCTCM ilianzishwa na serikali za China na Malta mwaka 1994. Hadi sasa, timu 20 za zilizoundwa na madaktari wa China wapatao zaidi ya 100 ambao wametoa matibabu ya TCM kwa wagonjwa takriban 250,000 wa Malta.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma