

Lugha Nyingine
Kundi la kwanza la watalii ya nchi za ASEAN waingia bila visa katika Xishuangbanna, China (6)
![]() |
Wafanyakazi wa reli wakiwasaidia watalii kutoka Laos na Thailand kupita kizuizi cha tiketi kwenye stesheni ya reli ya Xishuangbanna katika Mji wa Jinghong, Eneo linalojiendesha la Kabila la Wadai la Xishuangbanna, Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China, Februari 18, 2025. (Xinhua/Chen Xinbo) |
KUNMING - Jumanne jioni, watalii 15 kutoka Thailand na Laos walitoka nje ya stesheni ya reli ya Xishuangbanna ya Reli ya China-Laos, wakilakiwa na hafla ya kunyunyuziwa maji na ngoma yenye shamrashamraa.
Watalii hao ni kundi la kwanza la watalii kutoka nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) kutembelea Eneo linalojiendesha la Kabila la Wadai la Xishuangbanna lililoko Mkoa wa Yunnan kusini-magharibi mwa China tangu kutekelezwa kwa sera mpya ya kuruhusu makundi ya watalii kutoka nchi za ASEAN kutembelea eneo hilo ambayo ni kivutio maarufu cha watalii mkoani Yunnan bila visa kwa hadi siku sita.
Wakati wa uwepo wao, watalii hao watafurahia mandhari ya mazingira ya asili ya Xishuangbanna, na kuonja ladha ya vyakula vya kienyeji na desturi za kikabila.
Sera hiyo mpya ya visa imekuwa ikitumika tangu Februari 10, ikilenga kuunga mkono utalii kusini magharibi mwa China. Pia inatarajiwa kupanua ufunguaji mlango, kuhimiza mawasiliano ya watu, na kuzidisha ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na ASEAN, Idara ya Taifa ya Uhamiaji ya China imesema katika taarifa.
Jiang Jie, naibu mkurugenzi wa ofisi ya utamaduni na utalii ya Xishuangbanna, amesema kuwa hatua hiyo itaongeza soko la utalii wa ndani zaidi na kwamba Xishuangbanna itaendelea kukuza vifaa vipya vya utalii na kuboresha miundombinu yake ili kukidhi mahitaji ya watalii kwa namna iliyoboreshwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma