Roketi ya kubeba satalaiti ya Long March-8A yakamilisha safari ya kwanza tangu iundwe (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 12, 2025
Roketi ya kubeba satalaiti ya Long March-8A yakamilisha safari ya kwanza tangu iundwe
Kundi la satalaiti za obiti ya chini ya Dunia likirushwa ndani ya roketi ya kubeba ya Long March-8 iliyorekebishwa kutoka Eneo la Kurushia Satalaiti kwenda Anga ya Juu la Wenchang, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Februari 11, 2025. (Picha na Zhang He/Xinhua)

BEIJING - Roketi ya kubeba satalaiti ya Long March-8A ya China imefanikiwa kufanya safari yake ya kwanza Jumanne saa 11:30 jioni (kwa saa za Beijing) na kuingia kwenye obiti yake iliyopangwa awali kwa mafanikio, ikipeleka kundi la satalaiti za obiti ya chini ya Dunia kwenda anga ya juu kutoka Eneo la Kurushia Satalaiti la Wenchang, Mkoani Hainan, kusini mwa China.

“Long March-8A imeundwa ili kukidhi mahitaji ya urushaji wa mitandao mikubwa ya kundinyota katika obiti ya kati na ya chini za Dunia,” amesema Song Zhengyu, msanifu mkuu wa Long March-8A katika Akademia ya Teknolojia ya Vyombo vya Kurushwa kwenye Anga ya Juu ya China (CALT).

"Pamoja na umbo lake la kimsingi la roketi ya kubeba satalaiti ya Long March-8 na umbo lake la sehemu mbalimbali za nyongeza, inaunda roketi za Long March-8," Song amesema.

Amebainisha kuwa roketi za Long March zina uwezo wa upakiaji wa tani 3, tani 5 na tani 7 kwenye obiti zinazolingana na jua, ikiongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa China wa kurusha mitandao ya satalaiti za obiti ya kati na chini ya Dunia.

Song ameeleza zaidi kuwa, Long March-8A kwa ubunifu hujumuisha kazi za muundo wa uungaji mkono wa satalaiti, fremu ya adapta na moduli ya chombo katika moduli yenye kazi mbalimbali, ikipunguza kwa mafanikio uzito wa roketi kwa kilo 200 na kuboresha ufanisi wake wa upakiaji.

Liu Lidong, msanifu mwingine katika CALT, amesema kuwa hatua ya mwisho ya roketi -- kutumia hidrojeni kimiminika na oksijeni kimiminika kama mafuta - ina sifa ya juu ya msukumo, ikiwezesha roketi kufikia msukumo mkubwa kwa kutumia kiasi kidogo cha mafuta.

Kikundi hicho cha satalaiti kilichorushwa kwa mafanikio kwenye obiti ni cha pili cha aina yake na kitaunda kundinyota la mtandao. Urushaji wa roketi hiyo ni safari ya 559 kwa roketi za kubeba satalaiti za Long March.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha