Xi Jinping afanya ukaguzi Shenyang, Liaoning kaskazini mashariki mwa China kabla ya Mwaka Mpya wa Jadi (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 24, 2025
Xi Jinping afanya ukaguzi Shenyang, Liaoning kaskazini mashariki mwa China kabla ya Mwaka Mpya wa Jadi
Rais Xi Jinping wa China akifahamishwa kuhusu hatua zinazochukuliwa za kuongeza huduma za umma na kufahamishwa maendeleo yaliyopatikana katika kuboresha maisha ya watu alipotembelea maeneo ya makazi katika Mji wa Shenyang, mji mkuu wa Mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China, Januari 23, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

SHENYANG - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), amefanya ukaguzi katika Mji wa Shenyang wa Mkoa wa Liaoning, kaskazini-mashariki mwa China jana Ahamisi kabla ya sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, ambayo ni sikukuu muhimu zaidi kwa watu wa China, na sikukuu hiyo ya mwaka huu itakuwa Tarehe 29 mwezi huu.

Rais Xi ametembelea soko la vyakula na maeneo ya makazi katika mji huo wa Shenyang, ambako amefahamishwa kuhusu utoaji wa bidhaa wakati wa sikukuu hiyo na hatua zinazowekwa ili kukidhi mahitaji ya kila siku ya wakazi na kuongeza huduma za umma, pia kufahamishwa hali ya maendeleo yaliyopatikana katika kuboresha maisha ya watu.

Katika zaidi ya miaka 10 iliyopita, Rais Xi, akiwa kiongozi mkuu wa Chama na nchi ya China, ameifanya kuwa desturi kutumia wakati akiwa pamoja na watu wa kawaida kabla ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha