

Lugha Nyingine
Rais Xi atembelea wakaazi walioathiriwa na mafuriko kaskazini mashariki mwa China (4)
SHENYANG - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), jana Jumatano katika hali ya kukabiliwa na baridi kali, aliwatembelea watu walioathiriwa na mafuriko katika kijiji kilichoko Mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China.
Rais Xi amefunga safari hadi katika Kijiji cha Zhujiagou cha Wilaya ya Suizhong ya Mji wa Huludao, kabla ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, ambayo itaangukia Januari 29 mwaka huu.
Mji huo wa Huludao ulikuwa moja ya miji iliyoathiriwa zaidi na mafuriko katika majira ya joto mwaka 2024.
Rais Xi amekagua upigaji hatua katika urejeshaji wa hali ya kawaida na ujenzi upya wa baada ya janga hilo.
Akitembelea wanakijiji ambao walihamia katika nyumba zao mpya muda mfupi kabla ya majira ya baridi kali kuanza, Rais Xi amewauliza kuhusu ubora wa nyumba hizo zilizojengwa upya na hali ya uhakikishaji wa maisha yao ya kila siku.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma