Kutembelea Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Kela kwenye Mto Yalongjiang, mradi mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme kwa nishati ya maji na ya jua duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 26, 2024
Kutembelea Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Kela kwenye Mto Yalongjiang, mradi mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme kwa nishati ya maji na ya jua duniani
Picha hii iliyopigwa kwa droni ikionyesha kituo cha kuzalisha Umeme kwa nishati ya jua cha Kela. (Picha na Xue Di/ Chinanews)

Desemba 23, mwandishi wa habari wa CNS alikwenda Tarafa ya Kela ya wilaya ya Yajiang katika eneo linalojiendesha la Kabila la Watibet wa Garze, Mkoa wa Sichuan, China, akitembelea kituo kikubwa zaidi cha kuzalisha umeme kwa nishati ya maji na ya jua duniani -- kituo cha Umeme cha Kela, mradi wa kipindi cha kwanza wa kuzalisha umeme kwa nishati ya maji na ya jua wa Yalongjiang.

Mashine za Kituo hiki zina uwezo wa kuzalisha umeme kwa kilowati 1,000,000, na wastani wa matumizi yake ya mwaka umefikia saa 1735, na wastani wa uzalishaji wa umeme umefikia bilioni 2 kWh kila mwaka. Ujenzi wa kituo hicho ulikamilika na kuanza kuzalisha umeme mwaka 2023. Baada ya kukamilika kwake, umeme unaozalishwa kila mwaka unaweza kuokoa tani 600,000 za makaa ya mawe na kupunguza utoaji wa dioksidi kaboni kwa zaidi ya tani milioni 1.6 kila mwaka. Hayo yote yatafanya kazi ya vielelezo vya kuongoza katika kufikia malengo ya "kufikia usawazishaji wa utoaji kaboni", kuboresha muundo wa nishati wa kitaifa, na kusaidia kujenga mfumo wa nishati za kisasa na za kijani, usio na kaboni, wa usalama na wenye ufanisi mkubwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha