Majengo ya kale yaliyohifadhiwa vizuri katika kijiji chenye umri wa miaka zaidi ya 400 mkoani Guangxi, China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 24, 2024
Majengo ya kale yaliyohifadhiwa vizuri katika kijiji chenye umri wa miaka zaidi ya 400 mkoani Guangxi, China
Mwanakijiji akiondoa magugu kwenye shamba la mboga za majani katika Kijiji cha Longteng, Wilaya inayojiendesha ya kabila la Wayao ya Jinxiu, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, Desemba 18, 2024. (Xinhua/Zhou Hua)

JINXIU (GUANGXI) – Kikiwa kinapatikana katika sehemu ya kati ya Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, Kijiji cha Longteng kinajivunia majengo 49 ya kale yaliyojengwa kwa mtindo wa Enzi za Ming (1368-1644) na Qing (1644-1911). Kuanzia mwisho wa Enzi ya Ming hadi sasa, kwa zaidi ya miaka 400, ukoo wa Liang umekuwa ukistawi hapa, ambao umeshuhudia uwepo wa Vizazi 17 hadi sasa.

Mwaka 1620, familia ya Liang ilihamia hapa kutoka sehemu ya magharibi ya Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China. Likiangalia milima iliyofunikwa kwa mawe kama magamba ya dragoni, eneo hili linaonekana kama dragoni anayepaa. Kwa hiyo wanafamilia wa familia hiyo ya Liang waliliita eneo hili "Longteng" ikimaanisha dragoni anayepaa kwa Kichina, na kuishi hapa tangu wakati huo.

Likichukua eneo lenye ukubwa wa mita za mraba zaidi ya 20,000, kundi hilo la majengo ya kale katika kijiji hicho kwa sasa ndilo lililohifadhiwa zaidi na kubwa zaidi la Enzi za Ming na Qing katikati mwa mkoa huo wa Guangxi.

Kadiri hali ya maisha inavyozidi kuboreshwa katika miaka ya hivi karibuni, maisha ya kitamaduni ya wanakijiji yamezidi kuwa tajiri, huku shughuli mbalimbali zikiingiza ustawi ndani ya kijiji hicho.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha