Maendeleo ya roboti yenye umbo la binadamu yastawi katika Eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao ya China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 16, 2024
Maendeleo ya roboti yenye umbo la binadamu yastawi katika Eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao ya China
Mfanyakazi akijaribu uwezo wa kutembea wa roboti yenye umbo la binadamu ya TORA-ONE katika kampuni ya sayansi na teknolojia mjini Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Juni 28, 2024. (Xinhua/Mao Siqian)

Katika miaka ya hivi karibuni, maeneo mbalimbali katika sekta ya roboti yenye umbo la binadamu, kuanzia vipengele vya msingi hadi mfumo, yamekuwa yakistawi katika Eneo la Ghuba Kuu hiyo. Kampuni nyingi za teknolojia na taasisi za utafiti zimejitokeza hapa, zikiingiza akili na ujuzi zaidi katika ufanisi wa bidhaa za roboti yenye umbo la binadamu, ambazo hupelekwa hatua kwa hatua katika nyanja za uendeshaji wa viwanda, huduma za matibabu, elimu na utafiti, na nyinginezo. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha