

Lugha Nyingine
Mtaa wa Kisanaa wa Jinpifang, Shenzhen, China: Kiwanda cha zamani cha bia chakutana na Sanaa
Mtaa wa Kisanaa wa Jinpifang uko katika Wilaya ya Luohu, Mji wa Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, China. Uliwahi kuwa eneo la kiwanda cha awali cha bia cha Jinwei, ambacho kilikuwa kikijulikana sana kwa wenyeji wa Shenzhen. Hata hivyo, wakati wimbi la mageuzi na uboreshaji wa viwanda lilipokumba, Kiwanda hicho cha Bia cha Jinwei sasa hakifanyi tena kazi ya uzalishaji, kikiacha nyuma kiwanda kikubwa na vifaa.
Mwaka 2019, Timu ya Utafiti wa Desturi za Maisha ya Mijini ilianza kutumia tena mabaki ya Kiwanda hicho cha Bia cha Jinwei kulingana na uendelevu wa kijamii wa eneo husika. Eneo hilo la viwanda lililofanyiwa mageuzi makubwa ya kiubunifu lilifunguliwa kwa umma mwaka 2022 likiwa na sura mpya ya“Mtaa wa Kisanaa wa Kiwanda cha Bia”. Unachukua tamaduni za bia kama maudhui yake. Kwa msingi wa kuhifadhi majengo ya kihistoria ya uzalishaji bia, umeingiza vipengele vya kitamaduni, kisanii, na maisha, ukilipa eneo hilo kazi na hadhi mpya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma