Kijiji cha Uchoraji Picha kwa Kutumia Mafuta cha Dafen, Shenzhen, China: Jumuiya ya Sanaa katika Mji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 27, 2024
Kijiji cha Uchoraji Picha kwa Kutumia Mafuta cha Dafen, Shenzhen, China: Jumuiya ya Sanaa katika Mji
Picha za kuchorwa kwa mafuta za kuigilizia picha maarufu, “Heshima kwa Kazi Maarufu Mona Lisa” na “Heshima kwa Kazi Maarufu ya Picha ya Kujichorea ya Van Gogh”, ambazo zimechorwa na msanii wa Dafen. (Picha na Song Ge/People’ Daily Online)

Jana Jumatatu, Novemba 26, waandishi wa habari wa People’s Daily Online walifika Kijiji cha Uchoraji Picha kwa Kutumia Mafuta cha Dafen, kilichopo katika Mji wa Shenzhen, Mkoani Guangdong, China kutazama kazi mbalimbali za Sanaa zilizobuniwa na wasanii wenyeji, pia kujaribu kuchora picha hizo kwa kutumia mafuta chini ya usaidizi wa wasanii hao.

Kijiji cha Dafen kinajulikana kama “Kijiji No. 1 cha Uchoraji Picha kwa Mafuta nchini China” na kinapatikana kwenye Jumuiya ya Makazi ya Dafen ya Mtaa wa Buji mjini Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, China.

Katika siku za zamani, kijiji hicho kilikuwa kidogo cha kabila la Wahakka waliokuwa wakijishughulisha na kazi za kilimo. Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1980, kimevutia idadi kubwa ya wachoraji picha kwa kutumia mafuta kukusanyika. Kwa sasa Dafen kimekuwa kituo kikubwa zaidi cha uzalishaji na biashara ya picha hizo za kuchorwa kwa mafuta.

Takwimu zinaonesha kuwa, katika kipindi cha Dafen kuwa na pilika nyingi za kikazi na kibiashara, asilimia 70 ya picha za kuchorwa kwa mafuta katika soko la Ulaya zilitoka China, huku asilimia 80 ya kazi hizo zikitoka Kijiji hicho cha Dafen.

Kwa sasa Dafen inafanya juhudi za kuendana na zama za intaneti, ikihimiza muundo wa “intaneti”+uchumi na kunadi zaidi tasnia hiyo ya sanaa ya kijiji hicho kupitia matangazo ya moja kwa moja mtandaoni na njia zingine.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha