

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping wa China akutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (2)
![]() |
Asubuhi ya Tarehe 19, Novemba kwa saa za huko, Rais Xi Jinping wa China amekutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika wakati wa kuhudhuria kwenye Mkutano wa 19 wa kundi la nchi 20 (G20) huko Rio de Janeiro, Brazil. (Picha na Xie Huanchi/Xinhua) |
Rais Xi Jinping wa China amesema China na Ufaransa zina wajibu wa nchi kubwa wa kufanya jumuiya ya kimataifa kuwa na mshikamano ili kukabiliana na changamoto za kimataifa katika wakati ambao mabadiliko mengi mapya yanajitokeza katika mazingira ya kimataifa.
Xi ameyasema hayo alipokutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika wakati wa kufanyika kwa Mkutano wa Viongozi wa G20 huko Rio de Janeiro, Brazil. Ameeleza kuwa uhusiano kati ya China na Ufaransa una umuhimu wa kipekee wa kimkakati na ushawishi duniani kwani nchi zote mbili ni zinazojitawala, zilizokomaa na zinazowajibika, mwezi Mei mwaka huu, yeye na Macron walitoa matarajio juu ya miaka 60 ijayo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kutoa sauti kwa pamoja juu ya changamoto za kimataifa na matatizo makubwa mbalimbali, na kupata ushawishi duniani.
Kwa upande wake, Macron amesema Ufaransa inapenda kushirikiana na China kutekeleza kwa makini maoni ya pamoja yaliyofikiwa na marais wawili wa nchi, kuendelea kuimarisha mawasiliano kwenye ngazi ya juu, kuimarisha mawasiliano kati ya watu, kuendeleza urafiki wa jadi na kujenga uhusiano wa aina mpya kati ya nchi na nchi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma