

Lugha Nyingine
Meli ya kwanza ya China ya kuchimba kwenye kina kirefu cha bahari yaanza kufanya kazi (5)
GUANGZHOU - Meng Xiang, meli ya kwanza ya China inayosanifiwa na kuundwa nchini humo yenye uwezo wa juu wa uchimbaji wa kina cha kilomita 11 imezinduliwa rasmi katika mji wa Guangzhou, kusini mwa China jana Jumapili, ikiashiria hatua kubwa kufika mahali ambapo binadamu hajawahi kufikia hapo awali.
Ikiwa ni meli kubwa zaidi ya utafiti wa kisayansi ya China, Meng Xiang, ina urefu wa mita 179.8 na upana wa mita 32.8, na uzito wa tani 42,600. Inajivunia uwezo wa kusafiri maili 15,000 za baharini, uwezo wa kujitegemea kwa siku 120, na uwezo wa kubeba watu 180.
"Sampuli muhimu za chini ya baharini zitakazopata zitawapa wanasayansi wa kimataifa ushahidi wa moja kwa moja wa kuchunguza mpangilio wa magamba ya dunia, mabadiliko ya gamba la bahari, tabianchi za kale za baharini, na mipito mbalimbali ya maisha. “Itasaidia binadamu katika kuelewa, kulinda, na kutumia vyema bahari."
Chombo hicho ni cha kwanza duniani kujumuisha kazi kama vile uchimbaji wa kisayansi wa kina kirefu baharini, uchunguzi wa mafuta na gesi, na uchunguzi wa hidrati ya gesi asilia na uchimbaji wa majaribio.
“Baada ya raundi mbili za majaribio baharini, viashiria vyake muhimu vya ufanisi vimezidi matarajio ya muundo” amesema Zhang Haibin, mbunifu mkuu wa Meng Xiang amesema.
Amesema meli hiyo, ina kifaa cha kunyanyua majimaji cha kwanza duniani chenye uwezo wa kuchunguza mafuta na gesi na kuchukua sampuli kwenye kiini, kikiwa na uwezo wa juu wa kuinua tani 907.
Meli hiyo pia ina maabara tisa za hali ya juu, zinazojikita katika maeneo kama vile jiolojia, jiokemia, mikrobiolojia, sayansi ya bahari na teknolojia ya uchimbaji. Pia inajumuisha mfumo wa kwanza wa uhifadhi kiotomatiki sampuli za kiini zinazosafirishwa na meli ambazo zinaunga mkono utafiti wa baharini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma