

Lugha Nyingine
Kampuni za Tehama za China zaangalia soko la Afrika kwenye Tamasha la Teknolojia la Afrika 2024 (5)
![]() |
Watu wakitembelea mabanda ya kampuni za China kwenye maonyesho ya AfricaCom ya Tamasha la Teknolojia la Afrika, Africa Tech Festival 2024 mjini Cape Town, Afrika Kusini, Novemba 14, 2024. (Xinhua/Wang Lei) |
CAPE TOWN - Kampuni za mawasiliano ya simu za China, zilizoonyesha teknolojia na bidhaa vumbuzi katika Tamasha la Teknolojia la Afrika, Africa Tech Festival 2024 nchini Afrika Kusini, zimejiwekea malengo makubwa ya kupanua wigo wao katika soko la Afrika linalokua kwa kasi.
Likiwa limefanyika Novemba 12 hadi 14 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Cape Town katika mji mkuu wa kibunge wa nchi hiyo, tamasha hilo ambalo ni shughuli kubwa na yenye ushawishi mkubwa zaidi ya mawasiliano ya simu na teknolojia barani Afrika limevutia wahudhuriaji 15,000, waonyeshaji bidhaa zaidi ya 300, na wazungumzaji 450 kutoka bara zima na sehemu nyingine.
Kwa mujibu wa waandaaji wake, shughuli hiyo ilitoa "mtazamo wa nyuzi 360" wa namna uvumbuzi wa kiteknolojia na mabadiliko ya kimkakati yanavyounda upya sekta muhimu, huku pia ikitumika kama jukwaa la kuchunguza athari za kimageuzi za teknolojia katika sekta mbalimbali za Afrika.
Kampuni ya Mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya China Inspur., ikionyesha bidhaa zake kwa mara ya kwanza kwenye AfricaCom, mojawapo ya shughuli muhimu za tamasha hilo, imeonyesha matumaini kuhusu uwezekano wake wa ukuaji barani Afrika.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo katika eneo la Afrika Kusini mwa Sahara Sky Sun ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua: "Tunalenga kuvutia wateja zaidi siyo tu wa ndani bali kote katika nchi za Afrika za Kusini mwa Sahara."
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya China Unicom Kimataifa katika Kanda ya Afrika, Yao Siyang amesisitiza dhamira ya kampuni yake ya kupanua uwepo katika soko la Afrika, ikiwa ni mara yake ya nne kushiriki kwenye tamasha hilo.
"Tunafuraha kushiriki kwenye shughuli hii na kuleta suluhu zetu za kisasa kwa wateja wenyeji barani Afrika, ambapo tunaona uwezekano mkubwa wa ukuaji katika sekta ya mawasiliano ya simu na zaidi. Kuna fursa nyingi hapa, na tunaona kampuni mpya kuja kwenye bara hili kupanua biashara zao. Pia tunajivunia kuwa tunaweza kupata nafasi ya kuungana na kukutana na watu kwenye shughuli hii," Yao amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma