Chombo cha Shenzhou-18 cha kubeba wanaanga kwenye anga ya juu charudi duniani na kutua kwa mafanikio (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 04, 2024
Chombo cha Shenzhou-18 cha kubeba wanaanga kwenye anga ya juu charudi duniani na kutua kwa mafanikio
Chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-18 kilitua kwa mafanikio kwenye eneo la kutua la Dongfeng tarehe 4, Novemba. (Xinhua/Lian Zhen)

Saa saba na dakika 24 ya Novemba 4, Chombo cha Shenzhou-18 cha kubeba wanaanga kwenye anga ya juu kimerudi duniani na kutua kwa mafanikio. Madaktari wamethibitisha kuwa wanaanga watatu Ye Guangfu, Li Cong na Li Guangsu wako katika hali nzuri ya kiafya, na kuonesha kuwa jukumu la chombo cha Shenzhou-18 limepata mafanikio.

Chombo cha Shenzhou-18 cha kubeba wanaanga kwenye anga ya juu kilirushwa kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini Magharibi mwa China, Aprili 25, Mwaka 2024 na baadaye kimeunganishwa na kituo cha anga ya juu cha Tianhe. Wanaanga hao watatu walikaa kwenye obiti kwa siku 192, ambapo walifanya shughuli za nje ya chombo cha anga ya juu kwa mara mbili, na kuvunja rekodi ya muda wa wanaanga wa China kufanya shughuli za nje ya chombo cha anga ya juu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha