

Lugha Nyingine
Huawei yatoa mfumo wa HarmonyOS NEXT iliyouunda yenyewe (3)
![]() |
Yu Chengdong, mkurugenzi mtendaji wa Huawei, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa HarmonyOS NEXT mjini Shenzhen, Mkoani Guangdong, kusini mwa China, Oktoba 22, 2024. Xinhua/Bai Yu) |
SHENZHEN - Kampuni kubwa ya teknolojia ya China, Huawei imetoa HarmonyOS NEXT, mfumo wake endeshi wa programu (APPS) iliyouunda yenyewe bila kutegemea usanifu wa mfumo wa Android ambapo hafla ya uzinduzi mjini Shenzhen, makao makuu ya kampuni hiyo, inaashiria hatua nyingine muhimu kwa Huawei tangu Marekani kuiweka kwenye "Orodha ya Hatari kwa Usalama wa Taifa" mwaka 2019, ikiizuia kufanya biashara na kampuni za Marekani ikiwemo Google, ambayo hutoa Android.
HarmonyOS NEXT ni toleo la tano la mfumo wa HarmonyOS. HarmonyOS imeshafungwa kwenye vifaa zaidi ya bilioni 1, amesema Yu Chengdong, mkurugenzi mtendaji wa Huawei, katika hafla hiyo.
Yu amesema kuwa HarmonyOS NEXT inajitegemea kiukweli kutoka kwa Android na iOS ya Apple, ikiwa na mfumo endeshi, lugha ya programu, mfumokazi wa AI na vipengele vingine ambavyo vilitengenezwa bila kutumia mfumo endeshi wa Linux au msimbo wa chanzo wazi wa Android.
"HarmonyOS NEXT inatoa chaguo na nafasi mpya ya soko kwa ajili ya maendeleo ya sekta husika duniani kote," amesema, akiipongeza kuwa ni mfumo endeshaji ulio wazi, salama na wenye ufanisi.
Katika mwaka uliopita, Huawei imekuwa ikifanya kazi na washirika zaidi ya 10,000 wa ndani ya China kutengeneza programu za HarmonyOS NEXT, kusaidia kujenga mnyororo bunifu wa kiviwanda wa IT, Yu amesema.
Wataalamu wa sekta hiyo wanasema faida kubwa ya HarmonyOS ni uratibu wake wa majukwaa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na simu janja, magari na vifaa vingine vya teknolojia za akili bandia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma