

Lugha Nyingine
Msichana wa miaka 5 ashiriki ngoma ya jadi ya Yingge mkoani Guangdong, Kusini mwa China (7)
![]() |
Zhuang Enqi akicheza ngoma ya jadi ya Yingge na kikundi katika Kijiji cha Yujiao cha Tarafa ya Guiyu ya Mji wa Shantou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Mei 29, 2024. (Xinhua/Deng Hua) |
Ngoma ya jadi ya Yingge, yaani "ngoma na wimbo wa shujaa," ni aina ya ngoma ya jadi maarufu katika Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China ambayo inaunganisha opera, ngoma na sanaa ya Wushu. Ikiwa na historia ya kutokea Enzi ya Ming ya China ya kale (1368-1644), ngoma hiyo ya jadi mara nyingi huchezwa wakati wa sikukuu za jadi za Wachina. Ngoma hii ya Yingge iliorodheshwa kwenye kundi la kwanza la mali za urithi wa utamaduni usioshikika wa China Mwaka 2006.
Aprili 2024, video za msichana mwenye umri wa miaka 5, Zhuang Enqi, akicheza ngoma hiyo ya Yingge na kuchangamana na kikundi cha wacheza ngoma ya Yingge zilipata maoni ya mamilioni ya watu mtandaoni.
Baba yake Enqi, Zhuang Rongqiang, ni mpiga ngoma katika kikundi cha ngoma cha Yingge katika Kijiji cha Yujiao. Enqi mara nyingi alikuwa akienda kwenye ukumbi wa mazoezi wa kikundi hicho pamoja na baba yake na akajenga na kuendeleza shauku kubwa katika ngoma hiyo ya Yingge. Ngoma ndogo, matoazi, viunzi vya nyoka, na vijiti vya Yingge vilivyorekebishwa kwa ajili ya watoto viko kila mahali kwenye sebule ya familia ya Enqi. Wakati ngoma ya mvuto inapolia, Enqi huwa na umakini kila mara, akizungusha vijiti na kucheza akifuata midundo. Minyumbuliko yake changamfu, mizuri na yenye nguvu ya mwili huwafanya watazamaji wacheke na kupiga makofi mara kwa mara.
Huku kukiwa na kuongezeka kwa juhudi za mashirika ya eneo husika kuuleta urithi wa utamaduni usioshikika kwenye shule na jamii, vijana zaidi wanaanza kucheza ngoma ya Yingge na kuleta uhai mpya kwa aina hiyo ya mchezo wa sanaa wa kale.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma