China yarusha roketi ya kibiashara ya Gravity-1 kwenda anga ya juu kutoka baharini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 12, 2024
China yarusha roketi ya kibiashara ya Gravity-1 kwenda anga ya juu kutoka baharini
Roketi ya kibiashara ya kubeba vyombo kwenda anga ya juu ya Gravity-1 (YL-1) iliyobeba satelaiti tatu ikirushwa kutoka kwenye bahari karibu na pwani ya Haiyang, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, Januari 11, 2024. (Picha na Xinhua)

HAIYANG, Shandong – China imerusha roketi ya kubeba vyombo ya Gravity-1 (YL-1) kutoka baharini kwenda anga ya juu, ikituma satelaiti tatu kwenye obiti iliyopangwa katika anga ya juu ambapo Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Taiyuan kimerusha roketi hiyo ya kibiashara kutoka kwenye bahari karibu na pwani ya Haiyang, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, saa 7:30 Mchana. (Saa za Beijing).

Hii ni safari ya kwanza ya anga ya juu kwa roketi ya kibiashara ya YL-1 ya kubeba vyombo kwenda anga ya juu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha