Timu ya Madaktari wa China visiwani Zanzibar, Tanzania: Kunufaisha wenyeji kwa ustadi bora na moyo mwema (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 03, 2024
Timu ya Madaktari wa China visiwani Zanzibar, Tanzania: Kunufaisha wenyeji kwa ustadi bora na moyo mwema
Picha ikimwonesha daktari wa magonjwa ya wanawake Shi Xiaoying (kulia) akizungumza na daktari wa Pemba kuhusu hali ya wagonjwa wakati timu ya madaktari wa China ilipotoa huduma za matatibu bila malipo huko Pemba, Zanzibar. (Picha kwa hisani ya timu hiyo)

Septemba, 2023 timu ya 32 ya madaktari wa China kutoka Mkoa wa Jiangsu ilikuwa imekamilisha jukumu lao la mwaka mmoja na itarudi nyumbani China. Kwenye hafla ya kuwaaga madaktari hao, Mkurugenzi wa Hospitali ya Abdulla Mzee Bw. Rashid alisema kwa hisia kuwa, "Uhusiano kati ya madaktari wa China na madaktari na wauguzi wa Zanzibar umezidi ule wa urafiki, sisi ni ndugu, ni kaka na dada. Ninatumai urafiki wetu utadumu milele.”

Timu ya madaktari wa China visiwani Zanzibar ni timu ya pili ya madaktari ya kutoa msaada wa matibabu nje iliyotumwa na serikali ya China kwa Afrika. Mnamo mwezi Agosti, 1964, timu ya madaktari wa China ilifika Zanzibar, baada ya siku zaidi ya 10, tangu hapo China na Tanzania zimeanza kufanya ushirikiano wa matibabu ambao umeendelea kwa miaka 60.

Mwezi wa Septemba, 2022, timu ya 32 ya madaktari kutoka Mkoa wa Jiangsu, China ilifika Zanzibar kuanza kazi ya mwaka mzima ya huduma za matibabu. Kiongozi wa timu hiyo Zhao Xiaojun alisema, ili kutatua vizuri matatizo ya Wazanzibar ya kupata huduma za matibabu, timu hiyo hutumia wikendi na likizo kutoa huduma za matibabu bila malipo na kutoa dawa kwa wagonjwa wanaohitaji, hali ambayo imepokelewa vizuri na wakazi wa huko. Shughuli za kutoa huduma za matibabu bila malipo katika maeneo ya makazi zimefanyika zaidi ya mara 20. Ikijumuishwa na huduma hizo, timu hiyo imetoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa Zanzibar zaidi ya 60,000.

Sahal Juma mwenye umri wa miaka 24 alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye via vya uzazi na madaktari wa China. Alisema kwa furaha kuwa, “shukrani kwa madaktari wa China, sikuwahi kutarajia kwamba ningeweza kupata huduma bora ya matibabu karibu na nyumbani kwangu.”

Rais Mwinyi wa Zanzibar Tanzania alikutana na timu ya madaktari wa China mwezi wa Septemba mwaka jana, ambapo aliwatunukia madaktari hao wote medali za heshima na vyeti vya kumbukumbu, ili kusifu mchango uliotolewa na madaktari hao. Mwinyi alisema, teknolojia mpya na njia za matibabu ya kijadi ya China vilivyoletwa na timu hiyo vimesaidia Wazanzibar kuondoa maumivu na kulinda afya zao, na vimesaidia kuinua kiwango cha matibabu cha Zanzibar. “Shukrani kwa serikali ya China kwa msaada wake wa muda mrefu kwa maendeleo ya huduma ya afya ya Zanzibar.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha