

Lugha Nyingine
Senegal yazindua mtandao wa mabasi ya mwendokasi ya kutumia umeme kikamilifu ulio wa kwanza katika Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara
![]() |
Picha hii iliyopigwa tarehe 27 Desemba 2023 ikionyesha basi likiwa kwenye kituo cha mabasi cha mradi wa Mabasi ya Mwendokasi wa Dakar (BRT) mjini Dakar, Senegal. (Xinhua/Wang Zizheng) |
DAKAR - Senegal imezindua mtandao wa Mabasi ya Mwendokasi (BRT) ya kutumia umeme kikamilifu, ambao ni wa kwanza katika eneo la Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara katika mji mkuu Dakar, ambapo katika hafla ya uzinduzi, Waziri Mkuu wa Senegal Amadou Ba amesema kuwa mradi huo ni muundombinu wa kisasa sana, na pia ni uvumbuzi mkubwa.
Mradi huo wa mtandao wenye urefu wa jumla ya kilomita 18.3 na vituo 23 vya mabasi na vituo vitatu vikubwa vya abiria kubadili mabasi, umejengwa na Shirika la Barabara na Daraja la China (CRBC). Mabasi yote ya umeme kwa ajili ya mradi huu yametolewa na Shirika la Reli la Rolling Stock la China.
Baada ya kuzinduliwa kwa mtandao huo, muda wa kusafiri kutoka vitongoji vya Dakar hadi katikati ya mji huo utapunguzwa kwa nusu, na safari za watu mijini zitaboreshwa, amesema Huang Fei, meneja mradi wa CRBC.
Mradi huo ulitoa nafasi za ajira 1,500 wakati wa ujenzi na unatarajiwa kutoa nafasi za ajira zaidi ya 1,000 baada ya kuanza kufanya kazi, amesema Huang.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma