China yaendelea kuwa sehemu madhubuti kwa biashara za kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 22, 2023
China yaendelea kuwa sehemu madhubuti kwa biashara za kimataifa
Watembeleaji wa maonyesho wakiwa kwenye Maonyesho ya Uchumi wa Baharini ya China Mwaka 2023 (CMEE) mjini Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Novemba 23, 2023. (Xinhua/Liang Xu)

BEIJING - Mwaka mpya umekaribia na wafuatiliaji wa soko la kimataifa wanaudurusu Mwaka 2023 kwa China, mwaka wa kupata ushindi kwa mgumu, wenye kuimarika uchumi kwa hamasa huku kukiwa na hali ngumu ya kufufuka kwa uchumi wa Dunia. Licha ya changamoto za ndani na nje, China imeweza kusonga mbele na maendeleo yake yenye ubora wa juu, kutia nguvu eneo la Asia-Pasifiki na Dunia kwa ujumla kwa maendeleo yake thabiti, uwezo mkubwa na fursa nyingi sana.

Uchumi wa China umeshuhudia kuimarika kwa nguvu tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Pato la Taifa la China lilikua kwa asilimia 5.2 kwa mwaka katika robo tatu ya kwanza, na hivyo kuonyesha nguvu kubwa zaidi kati ya nchi zenye uchumi mkubwa duniani.

Steven Barnett, mwakilishi mkazi mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) nchini China, amesema kuwa China inaendelea kuwa injini kubwa zaidi ya ukuaji wa uchumi duniani Mwaka 2023, ikichangia theluthi moja ya ukuaji wa uchumi duniani.

"China inapokua kwa kasi, inatoa fursa ya ongezeko la uchumi inayokaribishwa na Dunia mzima," Barnett aliliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya awali.

Katika miaka ya hivi karibuni, China imefuata dhana mpya za maendeleo zenye uvumbuzi, uratibu, kijani, ya wazi na ya kunufaishana, na kujizatiti katika maendeleo yenye ubora wa juu. Ukuaji wa uchumi wa China umetoa matunda mengi na kuwa wa kijani zaidi, ukiingiza nguvu kubwa katika maendeleo endelevu ya kimataifa.

Wayne Huang, Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Biashara ya New Zealand, amesema kuwa China ni chanzo cha nguvu na nguzo ya utulivu wa maendeleo ya uchumi wa Dunia.

Mageuzi ya nishati ya China yametoa mchango mkubwa katika kuhimiza maendeleo endelevu duniani.

Waref Kumayha, Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo na Utafiti ya Njia ya Hariri nchini Lebanon amesema, China imekuwa na mchango chanya katika maendeleo endelevu ya dunia, na nchi nyingi zinatumai kujifunza kutokana na uzoefu wa maendeleo ya China na kujitahidi kwa pamoja kuwa na mustakabali mwema na mzuri.

Kujitolea kwa China katika kufungua mlango kwa kiwango cha juu kutanufaisha dunia nzima, amesema Jim Rogers, mwekezaji maarufu duniani na mchambuzi wa masuala ya fedha.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha