

Lugha Nyingine
Huduma ya Upelekaji Oda za Mizigo na Chakula kwa Droni katika maeneo ya chuo kikuu yaanzishwa Shenzhen, China
Huduma ya kwanza ya upelekaji oda za mizigo na chakula kwa droni katika chuo kikuu imeanzishwa siku ya Jumanne, Desemba 19, kwenye kampasi ya Shule ya Kimataifa ya wanafunzi wa shahada ya uzamili ya Shenzhen ya Chuo Kikuu cha Tsinghua iliyoko Shenzhen, China. Kwa mujibu wa habari husika, migahawa inayotoa huduma hiyo iko kwenye eneo la kibiashara lililoko umbali wa kilomita 2.6 kutoka kwenye kampasi hiyo. Wanafunzi wanapooda vyakula kutoka kwenye migahawa ambayo imeunganishwa na jukwaa la kuoda mtandaoni, wanaweza kuchagua kupokea oda zao kwa kupitia droni kufika sehemu iliyopangwa ndani ya kampasi. Kwa kawaida, vyakula hivyo hufika kwenye kampasi ndani ya dakika 5 hadi 6 baada ya kufungashwa. Kwa sasa migahawa iliyounganishwa na jukwaa hilo la mtandaoni ni pamoja na migahawa ya vyakula vya haraka, chai, kahawa n.k.
Picha na Mao Siqian/Xinhua
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma