

Lugha Nyingine
Kiwanda cha Akili Bandia chaboresha ubora na ufanisi wa uzalishaji bidhaa katika Mji wa Taizhou, Zhejiang, China
![]() |
Mfanyakazi akifanya kazi kwenye mstari wa uzalishaji bidhaa wa kiwanda kinachotumia teknolojia za akili bandia. (Picha na Zhang Yongtao/Tovuti ya Gazeti la Umma) |
Siku za hivi karibuni, kwenye mstari wa uzalishaji wa makasha ya mashine za kushona nguo wa kiwanda kinachotumia teknolojia za akili bandia cha Ghuba ya Taizhou cha Kampuni ya Teknolojia ya Jack, mikono ya roboti zinazotumia akili bandia ilikuwa ikizalisha kasha moja katika kila dakika.
Kwa mujibu wa habari iliyotolewa, mstari huo wa uzalishaji wa kampuni hiyo unatumia makumi ya maelfu ya vihisi, kwa kupitia vihisi na vidhibiti kubadilishana maelekezo na kuunganisha kwa urahisi, kampuni hiyo inawezesha uzalishaji wa kiotomatiki kwenye karakana. Kazi ambayo awali ilihitaji watu 300 sasa inaweza kukamilishwa na watu 10 tu. Ufanisi wa uzalishaji na kiwango cha matumizi ya nishati cha kampuni hiyo vimeboreshwa sana, na mzunguko wa ubunifu hadi uzalishaji wa bidhaa umefupishwa kwa 30%.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma