

Lugha Nyingine
Viwanda vinavyotumia teknolojia ya akili bandia vyachangia maendeleo ya tasnia ya machungwa huko Jiangxi, China (7)
![]() |
(Picha na Zhu Haipeng/People's Daily Online) |
Wafanyakazi wakikagua na kufungasha machungwa mabichi kwenye karakana inayotumia teknolojia ya akili bandia ya kampuni ya kusindika machungwa iliyoko ndani ya Eneo Maalum la Viwanda vya Teknolojia ya Hali ya Juu katika Wilaya ya Xinfeng, Mji wa Ganzhou, Mkoa wa Jiangxi, China, Tarehe 25, Novemba.
Katika miaka ya hivi karibuni, Mji wa Ganzhou katika Mkoa wa Jiangxi, China umekuwa ukifanya juhudi kubwa kutekeleza hatua za maendeleo yenye ubora ya tasnia ya machungwa. Kampuni nyingi za kusindika machungwa zinatumia teknolojia mpya ya “Intaneti ya Viwanda ya 5G+” na mistari mipya ya uzalishaji ili kufanya usindikaji wa matunda unaotumia teknolojia za kisasa, ikisaidia kuboresha ubora wa bidhaa za matunda na kuwezesha maendeleo yenye ubora wa hali ya juu ya tasnia ya machungwa huko.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma