

Lugha Nyingine
Misri yaandaa maonyesho ya TEHAMA ili kuwezesha mageuzi ya kidijitali (2)
![]() |
Watu wakitembelea banda la kampuni kubwa ya teknolojia ya China, Huawei kwenye Maonyesho ya TEHAMA ya Cairo Mwaka 2023 mjini Cairo, Misri, Novemba 21, 2023. (Xinhua/Ahmed Gomaa) |
CAIRO - Misri imeandaa Maonyesho ya 27 ya TEHAMA ya Cairo Mwaka 2023 yenye kaulimbiu isemayo "Kuchochea Uvumbuzi: Kuunganisha Akili na Mashine kwa ajili ya Dunia Bora Zaidi", ambayo ni maonyesho makubwa zaidi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) nchini humo, wakati nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika inataka kuwezesha mageuzi ya kidijitali kupitia kupata fursa za biashara za kunufaishana.
Maonyesho hayo yaliyofanyika kwa siku nne yamehitimishwa siku ya Jumatano katika Cairo Mpya, mji ulioko kusini mashariki mwa mji mkuu, Cairo. Yameweza kuonyesha maendeleo yaliyopatikana katika teknolojia ya habari, mawasiliano ya simu, mawasiliano ya satelaiti, na akili bandia, kwa mujibu Trade Fairs International, mratibu wa maonyesho hayo.
Maonyesho hayo yalilenga kuangazia jinsi teknolojia za akili bandia, zinapounganishwa na akili ya binadamu, zinavyoweza kuunda upya Dunia kupitia nguvu zake za kuleta mageuzi.
Kampuni zaidi 500 kutoka kote duniani zilishiriki kwenye maonyesho hayo ambayo yamevutia watembeleaji zaidi ya 100,000, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mratibu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma