

Lugha Nyingine
Maonyesho ya Uchumi wa Baharini ya China yafunguliwa, yakiangazia mafanikio ya tasnia hiyo (3)
SHENZHEN - Maonyesho ya Uchumi wa Baharini ya China Mwaka 2023 yenye kaulimbiu ya "kufungua Ushirikiano na Kunufaishana” yameanza siku ya Alhamisi katika mji wa Shenzhen, Kusini mwa China yakionyesha mafanikio mapya, sayansi na teknolojia ya hali ya juu, na ushirikiano wa kimataifa katika tasnia ya baharini ya China.
Yakiwa yamepangwa kufanyika kwa siku tatu maonyesho hayo ambayo yanachukua eneo lenye ukubwa wa kuvunja rekodi la mita za mraba 112,500 yamevutia kampuni, taasisi na mashirika 658 katika nyanja ya bahari kutoka nchi na maeneo 16, ikiashiria ongezeko la asilimia zaidi ya 60 kuliko mwaka jana wakati kama huo.
Yanatarajiwa kuonyesha hali za matumizi yenye uvumbuzi na teknolojia mpya na bidhaa mpya katika sekta kama vile uhandisi wa bahari na habari ya kielektroniki ya baharini.
Maonyesho hayo pia yatafanya makongamano ya kitaaluma zaidi ya 20, ambapo wageni zaidi ya 200 wa kimataifa kutoka nyanja za siasa, wasomi na biashara watafanya mijadala ya nje ya mtandaoni kuhusu sayansi na teknolojia ya baharini, tasnia ya baharini, bandari na usafirishaji wa meli, ustaarabu wa baharini, usimamizi wa bahari, na mada nyingine.
Signe Brudeset, Balozi wa Norway nchini China na Mongolia, amehudhuria hafla ya ufunguzi wa maonyesho hayo ambapo amesema China ni mojawapo ya wenzi wakubwa wa biashara wa Norway barani Asia, na maonyesho hayo yanatoa jukwaa zuri kwa kampuni nyingi za Norway kuwasiliana na wenzao wa China na kuimarisha mabadilishano na ushirikiano, ili kukuza biashara kati ya Norway na China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma