Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Mkutano wa Mtandao wa Intaneti Duniani Mwaka 2023 (WIC) wafunguliwa Mashariki mwa China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 09, 2023
Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Mkutano wa Mtandao wa Intaneti Duniani Mwaka 2023 (WIC) wafunguliwa Mashariki mwa China
Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Mkutano wa Mtandao wa Intaneti Duniani Mwaka 2023 (WIC) ukifunguliwa huko Wuzhen, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Novemba 8, 2023. (Xinhua/Huang Zongzhi)

HANGZHOU - Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Mkutano wa Mtandao wa Intaneti Duniani Mwaka 2023 (WIC) wenye kaulimbiu ya "Kujenga Dunia ya Kidijitali iliyo Jumuishi na Himilivu Yenye Manufaa kwa Wote -- Kujenga Jumuiya yenye Mustakabali wa Pamoja katika Mtandao wa Intaneti," na ukiwa na majukwaa madogo 20 yanayohusu mada za uchumi wa kidijitali, akili bandia, usalama wa mtandaoni na kadhalika, umeanza Jumatano katika mji wa kale wa maji wa Wuzhen katika Mkoa wa Zhejiang Mashariki mwa China.

Ripoti kuhusu China na maendeleo ya mtandao wa intaneti duniani, tuzo za vinara wa sayansi na teknolojia, na mifano bora ya kujenga kwa pamoja jumuiya yenye mustakabali wa pamoja katika nafasi za mtandao wa intaneti zitatolewa kwenye mkutano huo wa mwaka huu utakaoendelea hadi Ijumaa wiki hii.

Mkutano huo wa mwaka huu pia unaangazia shughuli mpya ikiwa ni pamoja na utoaji wa vyeo vya heshima na uzinduzi wa programu ya kimataifa ya uongozi wa vijana chini ya mfumo wa WIC.

Mwaka 2023 ni maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mkutano wa WIC wa Wuzhen. Tangu Mwaka 2014, mkutano huo umekaribisha washiriki karibu 12,000 kutoka nchi na maeneo 172.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha