Rais Xi Jinping asema China na Australia zimechukua njia sahihi ya kuboresha uhusiano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 07, 2023
Rais Xi Jinping asema China na Australia zimechukua njia sahihi ya kuboresha uhusiano
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Novemba 6, 2023. (Xinhua/Ding Haitao)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amekutana na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese mjini Beijing siku ya Jumatatu, akisema China na Australia zimeanza njia sahihi ya kuboresha uhusiano wao wa pande mbili.

"Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kufanyika ziara ya Waziri Mkuu wa Australia Gough Whitlam. Ziara yako ni safari ya kurejea historia na kupanga siku zijazo. Kutokana na juhudi za pamoja za pande zote mbili, China na Australia zimeanza tena mabadilishano katika nyanja mbalimbali na kuanza njia sahihi ya kuboresha uhusiano kati yao," Rais Xi amemwambia Albanese.

Huku akisema China na Australia zote ni nchi za Asia na Pasifiki na wanachama muhimu wa Kundi la nchi 20 (G20), hazina historia ya kukandamizana au migongano ya kimsingi ya kimaslahi, Rais Xi amesema kwa mtazamo wa maslahi binafsi, Dunia ni ndogo na imejaa, ikiwa na hatari na ushindani muda wote. Kwa mtazamo wa mustakabali wa pamoja, Dunia ni kubwa na pana, yenye fursa na ushirikiano kila mahali.

Amesisitiza kuwa hivi sasa, uchumi wa Dunia unakabiliwa na hali ya kukosa uthabiti, kutokuwa na uhakika na isiyotabirika, na uchumi wa nchi mbalimbali unakabiliwa na changamoto kubwa. Huku ukikabiliwa na mazingira magumu ya nje, uchumi wa China umehimili shinikizo, kuimarisha ukubwa wake, na kuboresha sifa yake.

"Maendeleo ya China bado yana msingi mzuri na hali nyingi nzuri. Kwa maendeleo yake thabiti, China italeta uhakika kwa uchumi wa Dunia usio na uhakika. China haiwezi kujiendeleza kwa kujitenga na Dunia, na Dunia inahitaji China kwa maendeleo yake," Rais Xi amesema huku akionya juu ya mwenendo wa kujenga “ua ndogo, uzio mrefu”, “kujitenga kiuchumi na kukata minyororo ya viwanda na ugavi” au “kuondoa hatari” ambapo ameuelezea kuwa ni kujihami kiuchumi na kwenda kinyume na uchumi wa soko huria.

Kwa upande wake Albanese amesema ni heshima kubwa kufanya ziara rasmi nchini China katika wakati huu wa kihistoria wa maadhimisho ya miaka 50 tangu kufanyika ziara ya Whitlam nchini China.

Amesema Katika miaka ya hivi karibuni, China imepata mafanikio makubwa katika kupunguza umaskini na kujiletea maendeleo. Na kwamba Australia na Dunia zimenufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na maendeleo ya muda mrefu, thabiti na endelevu ya China.

Albanese amesema pande hizo mbili zinapaswa kuheshimiana, kuwa sawa na kunufaishana, kuendelea na mawasiliano, kuimarisha maelewano na ushirikiano, na kupata matokeo yenye manufaa kwa pande zote.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha