Kundi la 40 la Utafiti wa Kisayansi katika Bahari ya Antaktika la China laanza safari (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 02, 2023
Kundi la 40 la Utafiti wa Kisayansi katika Bahari ya Antaktika la China laanza safari
Wafanyakazi wakitayarisha ngazi ya meli ya utafiti ya kuvunja barafu, Xuelong 2 kwenye kituo cha gati mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Novemba 1, 2023. (Xinhua/Zhang Jiansong)

SHANGHAI - Kundi la 40 la Utafiti wa Kisayansi katika Bahari ya Antaktika la China, ambalo ni ujumbe wa kwanza wa China wa kufanya utafiti wa kisayansi katika Bahari ya Antaktika kwa kutumia meli tatu limeanza safari yake Jumatano asubuhi, na kuanza kazi ya miezi zaidi ya mitano, ambapo meli za utafiti za kuvunja barafu za Xuelong na Xuelong 2, au Snow Dragon na Snow Dragon 2, zimeondoka kutokea mjini Shanghai, huku meli ya mizigo ya Tian Hui ikiondokea Mji wa Pwani wa Zhangjiagang katika Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China.

Timu hiyo ambayo inajumuisha wataalam zaidi ya 460, itachunguza athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye mfumo wa ikolojia wa Bahari ya Antaktika, pamoja na umuhimu wa Bahari ya Antaktika katika mabadiliko ya tabianchi. Watashirikiana na wenzao wa Norway na Australia kwenye miradi ya utafiti wa hali ya juu.

Kituo kipya cha utafiti wa kisayansi kitaanzishwa kwenye maeneo ya mwambao wa Bahari ya Ross wakati wa safari hii, na kuwa kituo cha tano cha utafiti cha China katika Bahari ya Antaktika na cha tatu cha kudumu, baada ya vituo vya Changcheng na Zhongshan.

Usanifu wa jengo la kituo hicho umehamasishwa na kundinyota la Crux lililokuwa likimuongoza mwanabaharia wa kale wa China Zheng He katika safari zake. Kikiwa na nafasi ya sakafu yenye ukubwa wa mita za mraba 5,244, kituo hicho kitaweza kusaidia wataalamu 80 wa kundi la utafiti kwenye safari za wakati wa majira ya joto na wataalam 30 wakati wa majira ya baridi kali.

Kituo hicho kitatumia kufuatilia na kuchunguza mazingira ya anga na baharini ya Bahari ya Antaktika pamoja na hali ya kibayolojia na ikolojia huko.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha