

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping afanya mazungumzo na mwenzake wa Colombia Petro, na kuinua uhusiano kati ya nchi zao kuwa ushirikiano wa kimkakati (5)
![]() |
Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo na Rais Gustavo Francisco Petro Urrego wa Colombia ambaye yuko ziarani nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Oktoba 25, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan) |
Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo mjini Beijing na Rais Gustavo Francisco Petro Urrego wa Colombia, ambaye anafanya ziara ya kiserikali nchini China, wakuu hao wawili wa nchi wametangaza kuinua uhusiano wa pande mbili kuwa ushirikiano wa kimkakati.
Rais Xi amesema tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia miaka 43 iliyopita, uhusiano kati ya China na Colombia umestahimili majaribu ya mabadiliko ya kimataifa na kudumisha kasi nzuri ya maendeleo.
Amesema pande hizo mbili zimeonyesha kuelewana na kuungana mkono katika masuala yanayohusu maslahi ya kimsingi ya kila mmoja na yanayofuatiliwa zaidi, zimepata maendeleo madhubuti katika maeneo mbalimbali, na kuimarisha urafiki kwa kudumu kati ya watu wa nchi hizo mbili.
Rais Xi amesema kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili ni matokeo ya juhudi za muda mrefu za sekta zote, na pia ni udhihirisho wa kuaminiana na kushirikiana kati ya pande hizi mbili, na kuongeza kuwa matokeo hayo yanapaswa kuenziwa na pande zote mbili na kuendelea kustawishwa na kuendelezwa.
Rais Xi amesema "China iko tayari kushirikiana na Colombia kuhamasisha ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Colombia ili kunufaisha zaidi watu wa nchi hizi mbili na kuingiza nishati chanya katika amani na maendeleo ya Dunia."
Ametoa wito kwa China na Colombia kuboresha muundo wa biashara baina ya nchi hizo mbili, na kuimarisha ushirikiano katika masuala ya habari, mawasiliano, uchumi wa kidijitali, biashara, mabadilishano kati ya watu na ya kitamaduni na ushirikiano wa pande mbili wa utekelezaji wa sheria na nyanja nyinginezo.
Rais Xi amesema uhusiano kati ya nchi hizo mbili unategemea usawa, kunufaishana na kupata matokeo yenye manufaa kwa pande zote. Pia ameikaribisha Colombia kujiunga na familia kubwa ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) mapema ili kufikia maendeleo na ustawi wa pamoja.
Rais Petro amesema Colombia iko tayari kuunganisha faida yake ya kijiografia na mikakati yake ya maendeleo na BRI, na kuimarisha ushirikiano katika miundombinu na nishati safi.
Pia amesema “Colombia iko tayari kudumisha mawasiliano na China kuhusu suala la Palestina na Israel, miongoni mwa mambo mengine, na kushinikiza kupatikana suluhu ya kusimamisha vita na kutuliza hali haraka iwezekanavyo,” na kuongeza kuwa Colombia inakaribisha Mapendekezo ya Maendeleo ya Dunia, Usalama wa Dunia na lile la Ustaarabu wa Dunia yaliyopendekezwa na Rais Xi, na iko tayari kuimarisha mawasiliano na uratibu na China ndani ya mifumo ya kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma