Mkutano Mkuu wa 13 wa Wanawake wa China wafunguliwa mjini Beijing (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 24, 2023
Mkutano Mkuu wa 13 wa Wanawake wa China wafunguliwa mjini Beijing
Mkutano Mkuu wa 13 wa Wanawake wa China ukifunguliwa kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Oktoba 23, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Beijing - Mkutano Mkuu wa 13 wa Wanawake wa China umefunguliwa rasmi siku ya Jumatatu kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China huku ukihudhuriwa na wajumbe karibu 1,800, wakiwemo wajumbe 90 walioalikwa maalum kutoka mikoa ya utawala maalum ya Hong Kong na Macao.

Saa 4 asubuhi, Rais Xi Jinping ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) na viongozi wengine waandamizi waliingia ukumbini na kupokelewa kwa makofi ya shangwe.

Shen Yueyue, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Watu wa China (CPPCC) na Mwenyekiti Mtendaji wa Tume Tendaji ya mkutano mkuu huo, alitangaza kufunguliwa kwa mkutano huo.

Akitoa hotuba kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC, Naibu Waziri Mkuu wa China, Ding Xuexiang ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC amepongeza mkutano huo kufunguliwa na kutoa salamu za ukarimu kwa wanawake na watu wanaofanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya wanawake kote nchini China pamoja na wanawake wenzao wa Mikoa ya Utawala Maalum ya Hong Kong na Macao na Taiwan, na wanawake wa China wanaoishi nchi za ng'ambo.

Katika hotuba yake, Ding ameangazia mchango mkubwa wa wanawake wa China tangu Mkutano Mkuu wa 12 wa Wanawake wa China.

Ameelezea uvumilivu na bidii ya wanawake katika kupunguza umaskini, harakati zao za kutafuta ubora katika uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, ushujaa wao katika kupambana dhidi ya janga la UVIKO-19, majukumu yao makini katika familia na jamii, kujitolea kwao katika kuhakikisha ufuataji wa sheria na taratibu, na mafanikio yao bora katika viwanja vya michezo.

"Jukumu muhimu la wanawake katika jamii limeonyeshwa kikamilifu, na maendeleo ya wanawake yameendelezwa kwa pande zote," Ding amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha