

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping akagua Mji wa Jiujiang katika Mkoa wa Jiangxi Mashariki mwa China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 12, 2023
NANCHANG - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amefanya ukaguzi katika Mji wa Jiujiang wa Mkoa wa Jiangxi, Mashariki mwa China siku ya Jumanne.
Rais Xi amekagua Bustani ya Utamaduni ya kitaifa katika eneo la Mto Changjiang la Mji wa Jiujiang na pia Kampuni ya Sinopec Jiujiang, ambapo alifahamishwa kuhusu juhudi za serikali za mtaa katika ujenzi wa bustani hiyo, urejeshaji wa ikolojia kando ya ufukwe wa Mto Changjiang, na mageuzi na maboresho ya kampuni ya petroli na kemikali ya Sinopec Jiujiang kuelekea maendeleo ya kijani.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma