

Lugha Nyingine
Roketi ya kibiashara ya China iliyobeba satelaiti 4 yarushwa kutoka baharini kwenda anga ya juu
HAIYANG, Shandong – China Jumanne imerusha roketi kwenye anga ya juu kutoka kwenye eneo la maji pembezoni mwa Haiyang, mji wa pwani katika Mkoa wa Mashariki wa Shandong, na kuweka satelaiti nne kwenye obiti iliyopangwa.
Roketi ya kibiashara iliyobeba satelaiti ya CERES-1, ilirushwa majira ya saa 11:34 jioni (kwa saa za Beijing). Kituo cha Urushaji Satelaiti kwenda Anga ya Juu cha Taiyuan kimeratibu safari hiyo kutoka baharini.
Watengenezaji wa roketi hiyo, Kampuni ya Galactic Energy imesema hiyo ni safari ya 9 na safari ya kwanza kutoka baharini kwa roketi za mfululizo za CERES-1. Urushaji huo pia unaifanya kampuni hiyo kuwa ya kwanza ya kibinafsi ya China kukamilisha safari kutoka baharini.
Ikilinganishwa na urushaji wa roketi kutoka kwenye ardhi, urushaji huo wa kutoka baharini ni hali mpya, ikiwa na kunyumbulika zaidi, uwezo bora wa kubadilika, na huduma za gharama nafuu zaidi. Zaidi ya hayo, uwekaji unaonyumbulika wa maeneo ya kurusha na ya kutua unaweza kuhakikisha hatua za roketi zilizotumika. Vifusi vingine huanguka baharini badala ya ardhini karibu na maeneo yenye watu wengi.
Faida hizi zinaipa kampuni hiyo ya roketi imani ya kuongeza mzunguko wa kurusha vyombo kwenye anga ya juu kutoka baharini katika siku zijazo.
Roketi hiyo ya CERES-1 iliyorushwa kwenye anga ya juu ilibeba setilaiti nne za Tianqi 21-24, zilizotengenezwa na Guodian Gaoke, kampuni ya kibiashara ya kisayansi yenye makao yake makuu mjini Beijing, ambayo ni sehemu ya kundi nyota la Mambo ya Intanteti la obiti ya chini ya Ulimwengu.
Kundinyota hilo la satelaiti 38 litaanza kufanya kazi Mwaka 2024. Litatoa huduma za data za kimataifa kwa matumizi ya programu kama vile mawasiliano ya dharura, ufuatiliaji wa mazingira ya ikolojia na kuhisi mawimbi ya minara.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma