Maonyesho ya Teknolojia za Kisasa ya China Mwaka 2023 (Smart China Expo 2023) yafunguliwa Chongqing, China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 05, 2023
Maonyesho ya Teknolojia za Kisasa ya China Mwaka 2023 (Smart China Expo 2023) yafunguliwa Chongqing, China
Watembeleaji wa maonyesho wakiangalia roboti kwenye banda la Ofisi ya Pili ya Uhandisi ya China katika Maonyesho ya Teknolojia za Kisasa ya China Mwaka 2023 (Smart China Expo 2023) yanayofanyika Mji wa Chongqing, Kusini-Magharibi mwa China, Septemba 4, 2023. (Xinhua/Wang Quanchao)

Maonyesho ya Teknolojia za Kisasa ya China Mwaka 2023 (Smart China Expo 2023) yamefunguliwa katika Kituo cha Maonyesho cha Kimataifa cha Chongqing, China siku ya Jumatatu.

Yakiwa yamepangwa kufanyika hadi siku ya Jumatano wiki hii, maonyesho hayo ya mwaka huu yanaangazia vyombo vya usafiri vinavyotumia nishati mpya vyenye teknolojia za kisasa, na vilivyoounganishwa na Mambo ya Intaneti. Yamevutia wadau wa biashara zaidi ya 500 kutoka ndani na nje ya China ili kuonyesha teknolojia zao za kisasa, bidhaa na matumizi katika viwanda vya teknolojia za kisasa na uchumi wa kidijitali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha