Rais Xi Jinping asema BRICS ni nguvu muhimu katika kuunda mazingira ya kimataifa (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 24, 2023
Rais Xi Jinping asema BRICS ni nguvu muhimu katika kuunda mazingira ya kimataifa
Rais Xi Jinping wa China, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Mkutano wa 15 wa Wakuu wa BRICS huko Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 23. 2023. (Xinhua/Li Xueren)

JOHANNESBURG - Rais Xi Jinping wa China amesema hapa siku ya Jumatano kwamba mfumo wa ushirikiano wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) ni nguvu muhimu katika kuunda mazingira ya kimataifa.

Rais Xi amesema kwenye Mkutano wa 15 wa wakuu wa BRICS kwamba, nchi za BRICS zichagua njia zao za maendeleo kwa kujitegemea, kutetea kwa pamoja haki yao ya maendeleo, na kusonga mbele kuelekea hali ya usasa, ambayo inawakilisha mwelekeo wa maendeleo ya jamii ya binadamu, na itaathiri sana mchakato wa maendeleo ya Dunia.

Amesema, historia ya BRICS inaonyesha kwamba nchi wanachama wake wamechukua hatua mara kwa mara kwa moyo wa BRICS wa uwazi, ushirikishwaji na ushirikiano wa kunufaishana, na kuupeleka ushirikiano wa BRICS kwenye viwango vipya katika kuunga mkono maendeleo ya nchi tano wanachama.

Ameeleza kuwa, nchi za BRICS zimeshikilia haki na usawa katika masuala ya kimataifa, kusimama kwa kile ambacho ni sahihi katika masuala makubwa ya kimataifa na kikanda, na kuongeza sauti na ushawishi wa nchi zenye masoko yanayoibukia na zile zinazoendelea.

“Nchi za BRICS hazibadilishi kanuni, hazisalimu amri kwa shinikizo kutoka nje, au kufanya kama vibaraka wa nchi nyingine,” amesema Rais Xi, na kuongeza kuwa zina maafikiano makubwa na malengo ya pamoja.

Rais Xi pia ameeleza kuwa nchi za BRICS zimekutana katika wakati muhimu ili kujenga juu ya mafanikio yao ya zamani na kufungua mustakabali mpya wa ushirikiano wa BRICS.

Ametoa wito kwa nchi wanachama wote kufuata mwenendo wa nyakati na kukaa mstari wa mbele huku akiongeza kuwa nchi zote za BRICS, zinapaswa kusaidia mageuzi ya utawala wa kimataifa ili kuufanya kuwa wa haki na usawa, na kuleta uhakika, utulivu na nguvu zaidi duniani.

Ametoa wito kwa nchi za BRICS kuwa marafiki wenza katika safari ya maendeleo na ustawishaji wa nchi, na kupinga utengano wa kiuchumi na usumbufu kwenye minyororo ya ugavi pamoja na umwamba wa kiuchumi.

Aidha, Rais Xi ametoa wito kwa nchi za BRICS kupanua ushirikiano wa kisiasa na usalama ili kudumisha amani na utulivu.

"Mtazamo wa Vita Baridi bado unasumbua Dunia yetu, na hali ya siasa za kijiografia inazidi kuwa mbaya," Rais Xi amesema.

Pamoja na masuala mengi ya kimataifa na kikanda aliyoyazungumzia, Rais Xi amesisitiza kuwa, sheria za kimataifa zinapaswa kuandikwa na kulindwa kwa pamoja na nchi zote kwa kuzingatia madhumuni na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, badala ya kuamriwa na wale wenye nguvu au sauti kubwa zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha