

Lugha Nyingine
Kuhisi mvuto wa teknolojia na kujistarehesha maisha ya likizo (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 23, 2023
![]() |
“Mashabiki wa teknolojia”wakitazama kwa makini roboti kuonyesha utaratibu wa kazi yake. (Picha na Wang Tianle/Tovuti ya Gazeti la Umma) |
Katika Maonesho ya Robiti ya Dunia, roboti nyingi za aina mpya zilionekana mbele ya watembeleaji, na kuvutia "mashabiki wengi wa teknolojia" kuzitembelea. Habari zinasema kwamba Maonesho ya Roboti ya Dunia ya kila mwaka hufanyika wakati wa likizo ya majira ya joto, na vijana na watoto kutoka sehemu mbalimbali nchini China wamekuwa watembeleaji wa kudumu kwenye maonesho hayo, ambapo wanahisi mvuto wa teknolojia kwa kupitia kutazama maonyesho na kuingiliana na roboti moja kwa moja.
Habari zinasema maonesho hayo ya Roboti ya mwaka huu yamevutia kampuni 160 za roboti za nchini na nje kuleta roboti zao karibu 600 kushiriki kwenye maonesho hayo, na kati ya hizo, roboti 60 za aina mpya zilionyeshwa kwa mara ya kwanza duniani.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma