Kilimo cha kidijitali chatoa mbegu za mafanikio vijijini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 17, 2023
Kilimo cha kidijitali chatoa mbegu za mafanikio vijijini China
Picha ikionesha kifaa cha GPS kilichofungwa kwenye mashine ya kilimo kinachowasaidia wakulima kupanda mahindi vijiji vya Tarafa ya Xinglongbao ya Wilaya ya Xinmin, Mkoa wa Liaoning wa China. (Picha ilitolewa na Kituo cha Vyombo vya Habari cha Xinmin.)

Hata katika msimu wenye pilikapilika zaidi za kilimo, Wang Shizhong, mkulima wa Kijiji cha Zhongguchengzi cha Wilaya ya Xinmin ya Mkoa wa Liaoning wa China, hakuwa na hangaiko lolote , kwa sababu alijua kila kitu kiko chini ya udhibiti kwa kupitia “MAP Kilimo, programu ya Akili Bandia” kwenye simu yake, ambayo inamwezesha kuangalia ramani ya satelaiti ya shamba lake, utabiri wa hali ya hewa kwa wakati halisi ndani ya saa mbili zijazo, na kiwango cha unyevunyevu wa udongo.

“Hapo zamani ilitubidi tupime shamba, kukagua mahitaji ya umwagiliaji na kusimamia hali ya ukuaji wa mazao sisi wenyewe . Lakini sasa satelaiti inatusaidia kukusanya data hizi, na mara moja kutuma ishara ya tatizo lolote na kubainisha sehemu ya tatizo husika. Ina Hii imetusaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa kazi ya kufanya doria shambani,” amesema Wang.

Katika miaka ya hivi karibuni, Wilaya Xinmin imekuwa ikisukuma kwa hamasa maendeleo ya “Kilimo cha Kidijitali” ili kusaidia kazi ya kulima na uzalishaji wa kilimo.

Hivi sasa Xinmin ina mabanda ya kilimo 55,000 hivi , ambayo kila mwaka uzalishaji wa mboga unafikia tani milioni 1. Xinmin inajitahidi kuanzisha kwa kila banda msimbo wa QR. Mbali na habari za upandaji mazao zilizohuishwa na wakulima, msimbo huo wa QR utakuwa na habari mbalimbali kuhusu alama za anuani za mabanda, ukubwa na umiliki wao.

Naibu Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Kilimo na Vijiji ya Xinmin Leng Zhuojian amesema “ habari hizi siyo tu zinasaidia katika uhakiki wa umiliki na usimamizi, bali pia zinawapa wakulima habari mbalimbali kuhusu shughuli za kilimo na ushauri wa masoko kupitia uchambuzi wa data kubwa”

“Siku hizi bei ya endive ni ya chini, kwa hivyo tutarekebisha halijoto ndani ya banda ili kuahirisha muda wa kupevuka kwa mazao ,” amesema mkulima Li Baoji, huku akibonyeza kitufe cha kushusha mapazia na kufungua mlango wa kupitisha hewa kitendo ambacho punde tu kilishusha halijoto ndani ya banda.

“Data kubwa itatoa usaidizi kwa kilimo cha mkataba, na kuongeza ubora wa mazao ya kilimo yatakayotolewa, ili kuongeza mapato ya wakulima” amesema Leng.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha