

Lugha Nyingine
Roketi ya Kuaizhou-1A ya China yarusha satelaiti tano mpya kwenya anga ya juu
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 15, 2023
XICHANG - China imefanikiwa kurusha roketi ya Kuaizhou-1A ambayo imebeba satelaiti tano mpya kwenye anga ya juu kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Xichang katika Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China siku ya Jumatatu.
Satelaiti za A hadi E zinazomilikiwa na Shirika la Satelaiti la Head-3 zimerushwa saa 7:32 Mchana (Kwa saa za Beijing), na imeingia kwenye obiti iliyopangwa kwa mafanikio.
Satelaiti hizo zitatumika hasa kwa kutoa huduma za kibiashara za kutambua kwa mbali.
Urushaji huo ni safari ya 27 kufanywa na mfululizo wa roketi za Kuaizhou-1A.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma