Treni ya kwanza ya mwendo kasi ya kilomita 350 kwa saa nchini China, yasafirisha abiria milioni 340 katika miaka 15 (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 02, 2023
Treni ya kwanza ya mwendo kasi ya kilomita 350 kwa saa nchini China, yasafirisha abiria milioni 340 katika miaka 15
Abiria wamepigwa picha kwenye kituo cha Beijing Kusini wakiwa ndani ya treni inayosafiri kati ya miji ya Beijing na Tianjin, Agosti 1, 2023. (Xinhua/Ju Huanzong)

Jumanne asubuhi treni namba C2551 iliondoka polepole kutoka kwenye kituo cha Beijing Kusini na kuelekea kwenye kituo cha Eneo jipya la Tianjin Binhai, na kuadhimisha mwaka wa 15 tangu kufunguliwa kwa reli ya kasi kwa treni inayosafiri kati ya miji ya Beijing na Tianjin.

Ikiwa ni reli ya kwanza kwa ajili ya treni ya mwendo kasi (HSR) yenye kasi kilomita 350 kwa saa nchini China, kwa ujumla reli ya kati ya Beijing na Tianjin imesafirisha abiria milioni 340 tangu ilipoanza kufanya kazi.

Takwimu kutoka Shirika la Reli la China tawi la Beijing zinaonesha kuwa, katika kipindi hicho cha miaka 15, safari za kila siku za treni zinazopata kwenye reli hiyo zimeongezeka kutoka 47 hadi 128, na muda mfupi zaidi wa kuondoka umefupishwa kutoka dakika 15 hadi dakika 3.

Hadi kufikia mwaka 2022, China ilikuwa na kilomita 42,000 za reli ya treni ya mwendo kasi ikiwa katika nafasi ya kwanza duniani, na hadi kufikia Juni 2022 urefu wa reli ya mwendo kasi inayofanya kazi mara kwa mara kwa treni yenye kasi ya kilomita 350 kwa saa, ulikaribia kilomita 3,200.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha