

Lugha Nyingine
Treni za “Reli ya Akili Bandia” zaanza uendeshaji wa majaribio ili kusaidia Michezo ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani huko Chengdu, China
Tarehe 25, Julai, treni mbili za kizazi kipya zinazotumia “teknolojia za akili bandia” zilianza uendeshaji wa majaribio wa kusafirisha abiria huko Chengdu, China. Treni hizo za kutumia teknolojia za akili bandia zinatoa huduma ya usafiri kwa umma ambayo ni safi, yenye kutoa kaboni chache na rafiki kwa mazingira, na zinasaidia wakazi wa huko kwenda uwanja wa Michezo ya 31 ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya FISU kwa ajili ya kutazama michezo, ambayo itaanza kufanyika huko Chengdu hivi karibuni.
Mfumo wa “Teknolojia za Akili Bandia” za reli hudhibiti kwa usahihi treni ili kuendeshwa kwenye reli iliyopangwa isiyoonekana kwa uhalisia kupitia maelekezo ya Kituo Kikuu cha udhibiti, na kasi ya treni hizo inaweza kufika kilomita 70 kwa saa. Hazihitaji kutandazwa kwa reli za kawaida zilizozoeleka na zinaweza kuendeshwa vizuri kwenye barabara za mijini.
Picha zimepigwa na Liu Zhongjun/Mwandishi wa Habari wa ChinaNews.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma