

Lugha Nyingine
Unataka kunywa kahawa? Ifikirie tu kisha unapata (2)
![]() |
Roboti inayoitwa "Xiao Fu" yenye uwezo wa "kusoma fikra akilini" kupitia kifaa cha EEG kinachoweza kutambua shughuli za ubongo. (Picha imetolewa na Chinadaily.com.cn) |
Chuo Kikuu cha Fudan kilichoko Shanghai, China kimezindua roboti ya akili bandia (AI) ambayo inawawezesha watu kuagiza kahawa kwa kuifikiria tu katika Mkutano wa Akili Bandia wa Kimataifa wa Mwaka 2023 huko Shanghai, Tarehe 7, Julai.
Roboti hiyo inayoitwa "Xiao Fu" inaweza "kusoma fikra akilini" kupitia kifaa cha EEG kinachoweza kutambua shughuli za ubongo. Pia ina uwezo wa kufuata amri za sauti kwa kutumia modeli ya lugha ya MOSS inayotegemea mazungumzo vilevile kutengeneza kahawa na kuiwasilisha kwa wateja.
"Kupitia usanidi wa programu na upangaji uwezo mbalimbali wa roboti za huduma kwa kutumia teknolojia za akili bandia, tunaweza kufikia hali mpya za kiakili bandia zinazounganisha wanadamu, mashine na vitu," amesema Peng Xin, Makamu Mkuu wa Shule ya Sayansi ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Fudan na kiongozi wa mradi huo wa roboti.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma