

Lugha Nyingine
Ndege ya Airbus iliyounganishwa sehemu zake nchini China yakabidhiwa kwa shirika la ndege la Ulaya
![]() |
Picha hii iliyopigwa Juni 27, 2023 ikionyesha ndege ya A321neo iliyokabidhiwa kwa Shirika la Ndege la Wizz la Hungary huko Tianjin, Kaskazini mwa China. (Xinhua) |
TIANJIN - Kampuni ya kuunda ndege ya Airbus, kwa mara ya kwanza, imekabidhi ndege iliyounganishwa sehemu zake na kukamilika katika mji wa Tianjin, Kaskazini mwa China kwa mteja wa Ulaya.
Shirika la Ndege la Wizz la Hungary, ambalo ni shirika kubwa zaidi linalotoa huduma kwa bei ya chini katika Ulaya ya Kati na Mashariki, limechukua ndege yake ya kwanza ya A321neo iliyounganishwa sehemu zake katika Laini ya Mwisho wa Kiwanda cha Airbus (FAL Asia) kwenye hafla iliyofanyika huko Tianjin Jumanne.
“Kukabidhiwa kwa ndege hii ni hatua muhimu kwa Airbus Tianjin,” amesema Christoph Schrempp, meneja mkuu wa Kituo cha Makabidhiano cha Airbus Tianjin.
Amesema kuwa, kutokana na hali ya kuimarika kwa uchumi wa China, FAL Asia imeendelea kuongeza uwezo wake wa kuunganisha sehemu za ndege, kusaidia kukidhi mahitaji ya wateja zaidi wa kimataifa na kuingiza msukumo mpya katika soko la anga la kimataifa.
Ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya ndege ya Airbus A321, kampuni hiyo ilitangaza mpango wake wa kupanua uwezo wa kiwanda chake cha FAL mjini Tianjin nchini China kuwa na kuzalisha aina ya A321 Mwaka 2021.
A321neo, ndege ambayo ni sehemu kubwa ya familia ya A320, inaweza kubeba abiria 244.
Kikiwa kilizinduliwa Mwaka 2008, Kiwanda cha FAL cha Tianjin kilikuwa laini ya kwanza ya kuunganisha sehemu za ndege za kibiashara za Airbus nje ya Ulaya. Tangu kukabidhi kwake kwa mara ya kwanza Ndege ya A320 Mwaka 2009, kiwanda hicho kimezalisha na kukabidhi zaidi ya ndege 600 katika kipindi cha miaka 14 tangu kianze kufanya kazi.
Mwezi Aprili mwaka huu, Kampuni ya Airbus ilitangaza ujenzi wa laini ya pili ya kiwanda cha kuunganisha sehemu za ndege huko Tianjin ili kupanua uwezo wa uzalishaji wa ndege A320 za abiria ili kukidhi mahitaji ya wateja wa kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma