Satelaiti zinazofadhiliwa na China zakabidhiwa kwa Misri (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 27, 2023
Satelaiti zinazofadhiliwa na China zakabidhiwa kwa Misri
Picha iliyopigwa Juni 25, 2023 ikionyesha modeli ya satelaiti ya kuruka angani iliyofungashwa ya mradi wa satelaiti ya MisrSat II kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika ofisi za Shirika la Anga ya Juu la Misri karibu na Mji Mkuu Mpya wa Utawala, Misri. (Xinhua/Wang Dongzhen)

CAIRO - Satelaiti mbili zinazofadhiliwa na China za mradi wa satelaiti wa MisrSat II zimekabidhiwa kwa upande wa Misri siku ya Jumapili, na kuifanya Misri kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuwa na uwezo wa kuunganisha sehemu, kukamilisha na kujaribu satelaiti.

Kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika ofisi za Shirika la Anga ya Juu la Misri karibu na Mji Mkuu Mpya wa Utawala, Misri, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Misri Rania Al-Mashat ameishukuru China kwa kuunga mkono na kushirikiana na shirika hilo, na kuwa "mshirika wa kimkakati na rafiki" wa Misri.

Amebainisha kuwa kituo cha MisrSat II cha satelaiti na kuunganisha sehemu zake na kukamilisha uundaji na majaribio (AIT) kinachofadhiliwa na China kimeongeza sana uwezo wa Misri katika utafiti na maendeleo, upimaji na udhibiti wa satelaiti, na kuifanya Misri kuwa nchi inayoongoza barani Afrika katika uwanja wa anga ya juu.

"Vifaa vya hali ya juu na teknolojia fanisi tuliyoona leo ni muhimu kwa Misri kwani inafungua mlango wa ushirikiano na Afrika katika uwanja huu," amesema.

Balozi wa China nchini humo Liao Liqiang amesema, ni mara ya kwanza kwa China kukamilisha majaribio makubwa ya satelaiti nzima nje ya nchi na kukamilisha na kukabidhi mradi wa ushirikiano wa satelaiti nje ya nchi.

"Misri ni nchi ya kwanza ya Afrika kuwa na uwezo kamili wa kuunganisha sehemu za satelaiti, kukamilisha uundaji na kufanya majaribio," Liao amesema.

Sherif Sedky, afisa mtendaji mkuu wa Shirika la Anga ya Juu la Misri, amesema katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, wahandisi na wataalam wa Misri na China wameshirikiana kuendesha kila hatua ya majaribio kwenye modeli tatu za satelaiti ya MisrSat II, zinazojumuisha modeli mbili za mfano na modeli moja ya satelaiti ya kuruka anga ya juu.

Amebainisha kuwa majaribio haya yamezindua kituo kikubwa cha satelaiti cha AIT barani Afrika na Mashariki ya Kati, ambacho kina vifaa kamili kupitia msaada kutoka China.

Baada ya kukabidhiwa kwa satelaiti hizo mbili za mfano huko Cairo, urushaji kwenye obiti wa modeli ya satelaiti ya kuruka anga ya juu ya MisrSat II pia umepangwa.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha