

Lugha Nyingine
Mazungumzo ya Nishan ya Mkutano wa Dunia wa Intaneti kuhusu Ustaarabu wa Kidijitali yafanyika mjini Qufu (5)
![]() |
Picha hii ya angani iliyopigwa Juni 26, 2023 ikionyesha mandhari ya nje ya ukumbi wa Mazungumzo ya Nishan ya Mkutano wa Dunia wa Intaneti kuhusu Ustaarabu wa Kidijitali huko Qufu, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Xinhua/Guo Xulei) |
BEIJING - Mazungumzo ya Nishan ya Mkutano wa Dunia wa Intaneti (WIC) kuhusu Ustaarabu wa Kidijitali yameanza Jumatatu huko Qufu, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, mahali alikozaliwa mwanafalsafa wa kale wa China, Confucius. (551 B.C.-479 B.K.)
Mazungumzo hayo yenye kaulimbiu ya "Zama za AI: Kujenga Dunia ya Kidijitali yenye Mawasiliano, Kujifunza kwa kila mmoja na Ujumuishi," ni shughuli ya kwanza inayoandaliwa na WIC ikiwa ni shirika la kimataifa.
Akihutubia kwenye hafla ya ufunguzi wa hafla hiyo, Zhuang Rongwen, mkurugenzi wa Idara ya Mtandao wa Intaneti ya China, amesema kuwa kuanzisha njia ya maendeleo ya Teknolojia za Akili Bandia (AI) inayoendeshwa na uvumbuzi, inayotegemea teknolojia, ya endelevu na yenye manufaa kumekuwa suala muhimu linalofuatiliwa na jumuiya ya kimataifa.
Zhuang amehimiza juhudi za kuchukua fursa za maendeleo ya AI, kutafuta na kuweka mikakati mizuri ya usimamizi wa AI, kuhimiza kwa pamoja mawasiliano na kujifunza kutoka kwa kila upande kati ya ustaarabu wa binadamu katika zama za AI, na kujenga kwa pamoja jumuiya yenye mustakabali wa pamoja katika mtandao wa intaneti.
Takriban wawakilishi 400 wa sekta mbalimbali duniani kote wameshiriki kwenye mazungumzo hayo mtandaoni au nje ya mtandao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma