Maonyesho ya Bidhaa za Akili Bandia Duniani 2023 yaanza kufanyika katika Mji wa Suzhou, Mkoa wa Jiangsu, China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 26, 2023
Maonyesho ya Bidhaa za Akili Bandia Duniani 2023 yaanza kufanyika katika Mji wa Suzhou, Mkoa wa Jiangsu, China
Maonyesho ya Matumizi ya Bidhaa za Akili Bandia Duniani 2023 ambayo yatafanyika kwa siku 3 yameanza kwenye Kituo cha Kimataifa cha Maonyesho cha Suzhou katika Mkoa wa Jiangsu nchini China, Juni 25, Mwaka 2023 na kuvutia watu wengi kutembelea na kupata uzoefu wa bidhaa hizo.

Maonyesho ya Matumizi ya Bidhaa za Akili Bandia Duniani 2023 ambayo yatafanyika kwa siku 3 yameanza kwenye Kituo cha Kimataifa cha Maonyesho cha Suzhou katika Mkoa wa Jiangsu nchini China Juni 25, Mwaka 2023.

Maonyesho hayo yanafuatilia zaidi teknolojia za Akili Bandia,ChatGPT, RPA+AI, kuendesha vyombo vya moto kwa akili bandia na kadhalika, na kuonyesha njia ya maendeleo ya kizazi kipya cha teknolojia za akili bandia. Katika kipindi cha kufanyika maonyesho hayo, kutakuwa na shughuli nyingine kama makongamano yenye mada mahususi, utoaji kwa umma wa bidhaa mpya, mwingiliano kati ya watu na teknolojia hizo na shughuli nyingine. (Que Mingfen/Tovuti ya Umma ya Picha)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha