China yaweka rekodi ya kurusha satelaiti 41 kwenye anga ya juu kwa kutumia roketi moja (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 16, 2023
China yaweka rekodi ya kurusha satelaiti 41 kwenye anga ya juu kwa kutumia roketi moja
Roketi ya Long March-2D iliyobeba satelaiti 41 ikirushwa kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Taiyuan, Mkoa wa Shanxi, Kaskazini mwa China Juni 15, 2023. (Zheng Bin/Xinhua)

TAIYUAN - China imerusha roketi ya Long March-2D kwenye anga ya juu kwa ajili ya kuweka satelaiti 41 kwenye obiti siku ya Alhamisi, na hii imeweka rekodi ya nchi ya China kurusha satelaiti nyingi kwa kurusha roketi moja tu.

Roketi hiyo ilirushwa saa 7:30 Mchana (Saa za Beijing) kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Taiyuan Kaskazini mwa China na punde kubeba satelaiti, ikiwa ni pamoja na satelaiti za Jilin-1 Gaofen 06A, kwenye obiti iliyopangwa mapema.

Hii ilikuwa safari ya 476 kwenye anga ya juu kwa roketi za mfululizo wa roketi ya Long March.

Satelaiti zilizobebwa na roketi hiyo zikiwemo pamoja na satelaiti 36 za Jilin-1 zilizoundwa na Kampuni ya Teknolojia ya Satelaiti ya Chang Guang, ambayo ni muundaji wa satelaiti za kibiashara katika Mkoa wa Jilin, Kaskazini Mashariki mwa China. Satelaiti hizo zitaongeza idadi ya satelaiti za Jilin-1 kwenye obiti hadi kufikia 108, na kukusanya kundi la satelaiti la kwanza la kibiashara la China lililoundwa na zaidi ya satelaiti 100 zenye uwezo wa kuhisi kwa mbali.

Kundi la kwanza la satelaiti za Jilin-1 lilirushwa Oktoba 2015. Katika miaka minane iliyopita, uzito wa kila satelaiti yenye kazi sawa umepunguzwa sana kutoka kilo 420 hadi kilo 22 pekee.

He Xiaojun, msanifu mkuu wa Jilin-1 Gaofen 06A, amesema kupunguza uzito kumenufaika kutokana na matumizi ya vihisi vya picha vilivyoboreshwa, mbinu bora za usanifu na chipsi za hali ya juu zilizounganishwa.

Amesema, mabadiliko hayo hayaathiri mwonekano wa picha za satelaiti bali kupanua safu zao zinazoonekana kwa asilimia 50. Pia zinapunguza gharama hadi moja ya ishirini ya satelaiti zilizorushwa zamani.

"Kama vile tu mabadiliko ya kompyuta," mwanasayansi huyo ameelezea, "kutoka kwenye kompyuta kubwa za mezani hadi kompyuta mpakato za kisasa na simu janja, vifaa vimepunguzwa ukubwa kwa sababu ya uboreshaji wa teknolojia, lakini ufanisi wa kompyuta unakuwa bora zaidi."

Kampuni hiyo imefahamisha kuwa, satelaiti hizo mpya zilizorushwa zitatumika katika kutoa huduma za data za kibiashara za kuhisiwa kwa mbali kwa sekta kama vile rasilimali za ardhi, uchunguzi wa madini na ujenzi wa miji ya kisasa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha