

Lugha Nyingine
Teknolojia za akili bandia zarahisisha shughuli za uwanja wa ndege kwenye Njia ya Hariri ya baharini huko Xiamen, China (2)
![]() |
Wafanyakazi wakifanya kazi na mfumo jumuishi wa utendakazi wa kidijitali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Xiamen Gaoqi huko Xiamen, Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China, Juni 12, 2023. (Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Xiamen Gaoqi/Xinhua) |
XIAMEN – Maendeleo ya kidijitali yanaharakisha maendeleo yenye ubora wa juu ya uwanja wa ndege wenye shughuli nyingi katika Mji wa Xiamen, Mashariki mwa China ulioko katika eneo la msingi la Njia ya Hariri ya Baharini ya Karne ya 21.
Teknolojia za kidijitali zimeunganishwa kikamilifu katika usimamizi wa usalama na uendeshaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Xiamen Gaoqi, ambao ni kituo muhimu cha usafiri wa ndege katika pwani ya kusini mashariki mwa China, kwa mujibu wa uwanja huo.
"Teknolojia za kidijitali zinawezesha uwanja wa ndege kuwa na mfumo jumuishi wa uendeshaji wa kidijitali ambao unaratibu usimamizi wa habari za usafiri wa ndege , magari yaliyoko nchi kavu na huduma, na sekta nyingine zinazohusika ," amesema Lin Zhenxing, Naibu Meneja wa Idara ya Usimamizi wa Habari ya Kampuni ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Xiamen Gaoqi.
Mji wa Xiamen unajitahidi kujenga kituo kinachounganisha Ukanda wa Kiuchumi wa Ukanda wa Kiuuchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri ya Baharini ya Karne ya 21, huku ukijenga ukanda wa kiuchumi uliounganishwa.
Ukiwa ni uwanja wa ndege wa msingi kwa mashirika manne ya ndege, Uwanja wa ndege wa Xiamen una njia ya kurukia ndege yenye urefu wa mita 3,400. Kabla ya UVIKO-19, Mwaka 2019, ulishughulikia hadi usafiri wa ndege wa kuruka na kushuka kwa mara 192,900, kuwasafirisha abiria milioni 27.41 na shehena za mizigo yenye uzito wa zaidi ya tani 330,000, na kuufanya kuwa uwanja wa ndege wenye njia moja ya kuruka ndege ulio na shughuli nyingi zaidi nchini China.
Meneja Lin amesema, teknolojia za kidijitali hivi sasa zinachangia mfumo wa jumla wa uendeshaji wa kidijitali wa uwanja wa ndege, na zinahusika na uratibu wa habari za usafiri wa ndege, huduma za magari uwanjani pamoja na usimamizi wa vitengo vingine husika.
Kwa kutumia kompyuta na simu za mkononi, mamlaka ya uwanja huo wa ndege na wafanyakazi wanaweza kuona kwa uwazi mienendo ya ndege ya wakati halisi, uendeshaji wa aproni na maelezo mengine ya uendeshaji, na kupokea tahadhari kwa wakati kuhusu hali isiyo ya kawaida.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma