China yarusha roketi ya kubeba mizigo ya Lijian-1 Y2 kwenye anga ya juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 08, 2023
China yarusha roketi ya kubeba mizigo ya Lijian-1 Y2 kwenye anga ya juu
Roketi ya kubeba mizigo ya Lijian-1 Y2 ikirushwa kwenda anga ya juu kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan Kaskazini-Magharibi mwa China, Juni 7, 2023. (Picha na Wang Heng/Xinhua)

JIUQUAN - China siku ya Jumatano imerusha roketi ya kubeba mizigo ya Lijian-1 Y2 yenye satelaiti 26 ndani yake kwenda anga ya juu.

Roketi hiyo iliruka saa 6:10 mchana (Saa za Beijing) kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan Kaskazini-Magharibi mwa China, na kutuma kundi la satelaiti za majaribio kwenye obiti iliyopangwa.

Setilaiti hizo zitatumika hasa kwa uthibitishaji wa teknolojia na huduma za kutoa habari za biashara za kuhisiwa kwa mbali.

Urushaji huo ni safari ya pili ya mfululizo wa modeli za roketi za kubeba mizigo za Lijian-1.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha