Kampuni ya China yaiundia Argentina treni ya kwanza inayotumia nishati mpya ya kuendeshwa kwenye reli nyepesi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 07, 2023
Kampuni ya China yaiundia Argentina treni ya kwanza inayotumia nishati mpya ya kuendeshwa kwenye reli nyepesi
Wageni kutoka Argentina wakipiga picha mbele ya treni ya kwanza inayotumia nishati mpya ya kuendeshwa kwenye reli nyepesi iliyoundwa na Kampuni ya CRRC Tangshan kwa ajili ya Argentina huko Tangshan, Mkoa wa Hebei, Kaskazini mwa China, Juni 6, 2023. (Xinhua/Gao Bo)

SHIJIAZHUANG – Kampuni ya CRRC Tangshan, muundaji mkuu wa treni za mwendo kasi wa China, imeunda treni ya kwanza inayotumia nishati mpya ya kuendeshwa kwenye reli nyepesi kwa ajili ya Argentina, ambayo ni mradi wa kwanza wa China kuuza treni kama hizo nje ya nchi.

Hafla ya kukamilika kwa uundaji wa treni hiyo imefanyika Jumanne huko Tangshan katika Mkoa wa Hebei, Kaskazini mwa China.

Treni hiyo yenye vyuma sita vya kushikilia magurudumu inakimbia kwa kasi ya juu ya kilomita 60 kwa saa ikiwa na uwezo unaonyumbulika wa kubeba abiria kuanzia 72 hadi 388. Ikiwa na vichwa pande zote mbili, treni hiyo inaruhusu kuendeshwa kwa pande mbili, amesema Luo Chao, meneja wa kiufundi wa mradi huo anayefanya kazi CRRC Tangshan.

Mwonekano wa nje na muundo wa rangi wa treni hiyo unatokana na Quebrada de Humahuaca, ambalo ni eneo la Urithi wa Dunia nchini Argentina, na muundo wa dirisha la kuwezesha kutazama nje hutoa urahisi mkubwa kwa watalii wa kutazama mandhari wanaposafiri kwa treni hiyo.

Ikiwa imewezeshwa kutumia nishati ya betri za lithiamu iron fosfati, treni hiyo itatumiwa na mfumo wa usafiri wa Jimbo la Jujuy nchini Argentina.

Zhou Junnian, Mwenyekiti wa CRRC Tangshan, ameeleza matumaini yake kuwa treni za China zinazotumia nishati mpya ya kuendeshwa kwenye reli nyepesi zitaongeza maendeleo ya utalii ya Jimbo la Jujuy la Argentina, na kujenga aina mpya ya ushirikiano wenye manufaa kati ya China na nchi za Latini Amerika. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha